Watu watano wakiwemo wanawake wanne na mwanaume mmoja ambaye ni dereva basi ndogo aina ya Toyota Hiache yenye namba za usajili T 962 BSE aliyetambuliwa kwa jina la Jackson Adam wamefariki dunia papo hapo baada yakugongana na basi la New force New lenye namba T 346 DLY likitokea Dar es Salaam kuelekea Tunduma na kusababisha majeruhi ya watu wengine tisa na kulazwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alithibisha kutokea kwa ajali hiyo Machi 4, mwaka huu majira ya saa nne asubuhi katika barabara kuu ya Morogoro – Iringa eneo la Lungemba – Rombo , Manispaa ya Morogoro kwa kuhusisha basi la aina ya Youtong lenye namba za usajili T 346 DLY mali ya kampuni ya New force.
Basi hilo lilikuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Tunduma na lilipofika eneo hilo liligongana uso kwa uso na basi ndogo aina ya Toyota Hiache yenye namba za usajili T 962 BSE ambayo lilikuwa likitokea kijiji cha Mlali, katika wilaya ya Mvomero kwenda Morogoro Mjini.
Kamanda Matei alisema katika ajali hiyo abiria watano waliokuwa ndani ya Toyota Hiache walifariki dunia papo hapo na wengine tisa kujeruhiwa na kukimbizwa hospitali ya Rufaa ya Morogoro kwa ajili ya kupatiwa matibabu na hakukuwa na majeruhi kutoka basi la New Force .
Kamanda wa Polisi wa huyo aliwataja waliofariki dunia ni pamoja na dereva wa basi dogo Jackson Adam ambaye ni mkazi wa Kata ya Chamwino, Manispaa ya Morogoro, na wengine wanawake Georgina Aloyce (35) , Revocatha Raymond Lyimo , Mangasa Almasi na Witness Leonard Mwamuni (26).
Pia aliwataja majeruhi waliokuwa kwenye basi dogo ni watoto wawili waliofiwa na mama yao katika ajali hiyo ambao ni Catharine Mhagama (6) na Caltimei Mhangama mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi miwili, Prisca Isaya (25), Chuki Wage (40), Anthon Cletus Mhando (39) mkazi wa eneo la SUA, Innocent Emilian , Willbrod Emilian ambao ni watu wazima mapacha , Iman Amri Salum na kondakta wa daladala hiyo Ally Ramadhan.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi huyo , chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi dogo ambaye ni marehemu kutaka kulipita lori la mchanga lililokuwa mbele yake bila kuchukua tahadhari na hivyo kugonaga na basi la Kampuni ya New Force ambalo lilikuwa likiendeshwa na Mdula Abdallah (52) mkazi wa Dar es Salaam. Hata hivyo alisema , Polisi inamshirikia dereva Mdula Abdallah wa Kampuni ya New Force kwa ajili ya uchunguzi zaidi kutokana na ajali hiyo.
Alisema ,mazingira ya ajali hiyo inaonesha huenda dereva wa basi hilo alikuwa katika mwendo kasi uliomsababishia ashindwe kupunguza mwendo mara baada ya kuona basi ndogo likilipita lori lililokuwa mbele ambapo ageweza kunusuru ajali hiyo mbaya iliyopoteza maisha ya watu isitokee
0 Post a Comment:
Post a Comment