Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka wanawake wote ambao wametelekezwa na waume zao na kubeba majukumu ya kulea watoto peke yao, wafi ke ofi sini kwake Aprili 9, mwaka huu kwa ajili ya kupatiwa msaada wa kisheria.
Alisema hayo juzi wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, ambayo kimkoa yalifanyika wilaya ya Ubungo. Alisema kumekuwa na ongezeko kubwa la wanawake, ambao wanalea watoto peke yao wakati wenza wao wapo, lakini hawatoi msaada wowote.
‘’Unakuta mwanamume anamsababishia mwanamke afukuzwe nyumbani kwa sababu ya kupata mimba, wengine wanafukuzwa na ndugu zao, wengine wanahangaika kulea watoto peke yao na mwanaume yupo. Hivyo nataka mfike ili muweze kupatiwa msaada wa kisheria,’’ alisema Makonda.

Alisema tayari ameshapitia sheria ya malezi na kuona matakwa ya sheria hiyo kwamba watoto wanapaswa kulelewa na wazazi wote wawili kwa kushirikiana; na sio kumuachia mzigo mama peke yake.
‘’Moyo wangu umebeba huzuni ya akina mama ambao wanateseka nataka mpate haki yenu ya malezi ninachowaomba wanawake endeleeni kuliombea Taifa, Rais na viongozi wengine wa serikali ili waendelee kuwasaidia kupata usawa wa kijinsia,’’ alisema Makonda.
0 Post a Comment:
Post a Comment