Maafisa nchini Tanzania wanasema kuwa wanatafuta suluhu ya kidiplomasia kuhusu kisa kinachohusisha Zambia, ambapo malori 600 ya Tanzania yamekamatwa na kuzuiliwa kwa kipindi cha miezi miwili.
Zamba iliyakamata malori hayo yalipokuwa yakirudi kutoka DR Congo ambapo yalikuwa yameenda kubeba mbao.
Rais wa Zambia Edgar Lungu siku ya Jumatatu alisema kuwa hatokubali taifa lake kutumika kama kituo cha miti ya mbao akidai kuwa madereva wa malori kutoka Tanzania wanakiuka sheria kuhusu usafirishaji mbao.
Maafisa wa Tanzania wametoa wito kwa maafisa wao katika ubalozi wao nchini Zambia kuwasilisha swala hilo na maafisa husika ili kupata suluhu ya haraka.
Muungano wa madereva wa malori wa Tanzania Tatao umesema kuwa wanachama wake walifuata maelezo yote kuhusu ununuzi na mauzo ya nje ili kuweza kuingia nchini DR Congo.
Tatao inasema kuwa wanachama wake wamapoteza zaidi ya dola milioni 6 katika miezi miwili ambayo madereva hao wamekamatwa.
Comment, like and share
0 Post a Comment:
Post a Comment