Dar es Salaam. Shirikisho la vyama vya wafanyakazi (Tucta) limeitaka serikali kusitisha makato ya asilimia 15 kama malipo ya mkopo wa elimu ya juu na kurudi kiwango cha awali cha asilimia nane kinyume na hapo wataipeleka mahakamani.
Rais wa Tucta, Tumaini Nyamhokya alisema Baraza kuu la shirikisho hilo limesharidhia uamuzi huo na tayari lipo kwa wanasheria.
"Wanasheria wetu wanalifanyia kazi na kuendelea kukusanya nyaraka zitakazotusaidia,muda wowote kuanzia wiki Idaho tutalifikisha suala hili mahakamani," alisema
Alisema ameendelea kupata malalamiko mengi kutoka kwa wafanyakazi kutokana na makato hayo ikilinganishwa na hali ngumu ya maisha ilivyo sasa.
0 Post a Comment:
Post a Comment