Waziri wa Utumishi, Angela Kairuki amemkabidhi Rais John Magufuli majina ya watumishi wenye vyeti feki huku akieleza kuwa waliobainika kughushi vyeti watahukumiwa kifungo cha miaka saba jela kulingana na kanuni za utumishi wa umma za mwaka 2016.
Kairuki amesema sheria hizo pia zinawaweka hatiani mawakala wote wanaotumika kutengeneza vyeti feki.
Amesema kanuni za utumishi wa umma za 2016, zinaeleza kuwa muombaji wa nafasi za ajira serikalini akitoa taarifa za uongo atachukuliwa hatua za kijinai na kinidhamu.
Mshirikishe Mwenzako: www.zakacheka.blogspot.com
0 Post a Comment:
Post a Comment