24 Mei 2017
Rais Duterte amekatiza ziara yake Urusi alikokuwa anakutana na rais Vladimir Putin
Vikosi vya usalama vimekuwa vikipiga doria baada ya kutangazwa kuidhinishwa sheria hiyo ya kijeshi Mindanao
Rais Durtete ambae ni mzaliwa na kisiwa cha Mindanao, ametangaza kuidhinishwa sheria hiyo ambayo huenda ikadumu kwa mwaka mmoja katika kukabiliana vikali na ugaidi.
Ghasia zilizuka katika mji wa Marawi ulio na wakaazi laki mbili wakati jeshi lilipoanza kumsaka kiongozi wa kundi la wapiganaji wa Maute ambao ni washirika wa kundi la Islamic State.
Taarifa zinasema wapiganaji wa Maute walikua wamethibiti hospitali kuu, gereza na kuteketeza majengo mengi yakiwemo makanisa.
Hali katika kisiwa cha Mindanao imelazimu Rais Rodrigo Durtete kukatiza ziara yake nchini Urusi ambapo ametaka nchi yake kupata silaha za kisasa kukabiliana na ugaidi baada ya kushauriana na mwenyeji wake Vladmir Putin.
Sheria ya kijeshi inaruhusu wanajeshi kuwashikilia washukiwa kwa muda mrefu bila kuwafungulia mashtaka.
Katiba ya Ufilipino inasema rais anaweza kutangaza sheria ya kijeshi kwa siku 60 kusitisha uasi au uvamizi.
Bunge linaweza kuifutilia mbali hatua hiyo katika muda wa siku mbili huku mahakama ya juu zaidi inaweza kukagua uhalili wa kuidhinishwa kwake.
Hii ndio mara ya pili sheria hii imewekwa Ufilipino tangu kuanguka kwa uliokua utawala wa Ferdinand Marcos mwaka wa 1986.
0 Post a Comment:
Post a Comment