Rais Kabila asema uchaguzi utafanyika mwishoni wa mwaka huu

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM=>
Rais Joseph Kabila amepinga ukosoaji unaotekelezwa na jamii ya kimataifa kuhusu kucheleweshwa kwa uchaguzi katika jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Katika mkutano na wanahabari kuadhimisha miaka 17 madarakani, aliahidi kwamba uchaguzi huo utafanyika mwisho wa mwaka huu.

Mkutano huo na vyombo vya habari mjini Kinshasa ulikuwa wa kwanza katika kipindi cha miaka mitano.Na ulichukua saa tatu.

Aliikosoa Monusco akisema ujumbe huo wa Umoja wa Mataifa hauko nchini DRC ili kuendesha shughuli za taifa hilo.

Katika shutuma dhidi ya muungano wa Ulaya na Marekani, ambao wamekosoa makabiliano dhidi ya waandamanaji, alisema: DRC sio koloni .Taifa hili lazima liheshimiwe.

Alionekana akilikumbusha kanisa katoliki akisema kuwa maandamano yanayofanywa na wakristo dhidi ya serikali yake yanafaa kuruhusiwa lakini waandalizi ni lazima washtakiwe.

Serikali hiyo hivi majuzi ilitangaza kwamba uchaguzi utafanyika tarehe 23 Disemba, ikiwa ni miaka miwili baada ya kukamilika kwa muda wa utawala wa rais huyo.

www.zakacheka.blogspot.com
www.zakachekainjili.blogspot.com
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: