Trump alaumiwa kwa kukataa Sheria kumiliki Silaha

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM=>
Chama cha Democrats kimewashutumu Rais Donald Trump na Spika wa bunge la nchi hiyo Paul Ryan kwa kukataa kuruhusu mjadala wa sheria ya kumiliki silaha.
Hii imetokea siku moja baada ya wanafunzi 17 kuuawa kwa kupigwa risasi huko Marekani.
Wakati huo huo shughuli ya kuwasha mishumaa kuwakumbuka waliouawa kwenye tukio hilo imefanyika huko Florida kulikotokea tukio hilo.
Wakati wa Marekani wakiwa bado wanaendelea kuomboleza kifo cha wanafunzi 17 waliuawa kwa kupigwa risasi kumekuwa na wito wa nchi hiyo kubadili sheria ya kumiliki silaha.

Rais Donald Trump akizungumza na waandishi wa habari baada ya shambulioHaki miliki ya pichaWIN MCNAMEE
Image captionRais Donald Trump akizungumza na waandishi wa habari baada ya shambulio

Akizungumzia mauaji hayo Rais wa Marekani Donald Trump awali katika hotuba yake amesema usalama katika shule utakuwa ni moja ya mambo yatakayopewa kipau mbele.
Hata hivyo alishindwa kulishauri bunge la nchi hiyo lipitie upya sheria ya kumiliki silaha.
"Utawala wetu unafanya kazi kwa karibu na mamlaka za eneo la mji kuchunguza tukio la kupigwa risasi na kupata taarifa zote iwezekanavyo. Tumejitolea kufanya kazi na jimbo pamoja na viongozi wa eneo hilo kusaidia kulinda usalama wa shule na kukabiliana na masuala magumu yanayotokana na matatizo ya afya ya akili." alisema Rais Trump
Siku ya Jumatano watu 17 waliuawa kwa kupigwa risasi na mwanafunzi aliyefukuzwa shule kwa utovu wa nidhamu katika shule moja huko katika jimbo la Florida.

Students hugging and cryingHaki miliki ya pichaAFP/ GETTY IMAGES
Image captionWanafunzi 3000 wa shule hio walikuwa wanamalizia siku yao wakati shambulio hilo lilipotokea

Akihutubia katika tukio hilo Baba wa mwanafunzi wa miaka 14 aliyeuawa kwenye tukio hilo Fred Guttenberg amesema familia yake imeumia kutoka na kifo mtoto wao.
"Haina maana. Hii haiwezekani. binti yangu , mtoto wangu mwenye umri wa miaka 14. na kwenu mnaojua binti yangu Jamie, alikuwa ni maisha katika burudani. Alikuwa anatutia nguvu tukiwa nyumbani.

Mtuhumiwa huyo akifika mbele ya mahakama kusikiliza mashtakaHaki miliki ya pichaPOOL
Image captionMtuhumiwa huyo akifika mbele ya mahakama kusikiliza mashtaka
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: