Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amezindua ndege inayojiendesha yenyewe bila ya rubani ambayo ni ya kwanza kutengenezwa nchini humo.
Kifaa hicho kilichotengenezwa na Taasisi ya Teknolojia ya jeshi la anga la Nigeria, kitatumika kupambana na wapiganaji pamoja na majambazi.
Mipango ya jeshi la nchi hiyo ni kutengeneza vifaa hivyo kwa wingi na pia uwezekano wa kuvisafirisha katika nchi nyingine.
Nigeria imekuwa ikikabiliwa na kitisho cha usalama, ikiwemo wapiganaji wa kiislamu walioko kaskazini mwa nchi hiyo, wapiganaji walioko katika eneo lenye utajiri wa mafuta, kusini mwa nchi na mapigano kati ya wafugaji na wakulima katika jimbo la kati mwa nchi hiyo.
0 Post a Comment:
Post a Comment