Rais wa China Xi Jinping ameitisha suluhisho la amani kuhusu taharuki iliyotanda Korea kaskazini, katika maongeo ya simu baina ya rais wa Marekani na Donald Trump, vyombo vya habari China vimesema.
Siku ya jumanne Trump aliandika kwenye mtandao wa kijamii tweeter kuwa Marekani haiogopi kupambana na Korea Kusini iwapo China haitasaidia.
Hali ya taharuki ilitanda katika rasi ya Korea kusini baada ya kupelekwa kwa meli za kivita kutoka marekani katika eneo hilo.
Korea kusini ilikasirishwa na hatua hii na ikajibu kwamba itajilinda vilivyo.
Bwana Xi na Trump walikutana ana kwa ana wiki jana katika mkutano mjini Florida ambapo waliongea kuhusu Korea kusini.
Mawasiliano yao ya simu yalifanywa jumatano asubuhi, kulingana na shirika la utangazi la China CCTV. White House bado haijatoa maelezo yoyote.
Katika maongeo yao, Bwana Xi alisema kuwa China imejitolea kulinda amani na utulivu kwenye rasi ya Korea kusini na imeunga mkono kutafuta suluhisho kwa njia ya amani, CCTV ilisema.
Mapema jumatano, tahariri zilizochapishwa na shirika la utangazaji la Global Times ilitoa mwito kwa Korea kusini isizingatie amani mwanzo, ikinukuu kwamba Marekani haina mpango wa kuishi vyema na Pyongyang ambayo inamejihami na silaha za kinuklia.
Trump alisema kuwa alimwelezea Rais wa China kwamba mkataba wa kibiashara na Marekani ina manufaa mazuri kwao iwapo watasuluhisha tatizo la Korea kusini.
Katika mahojiano siku ya Jumanne katika shirika la utangazaji la Fox Business Network Marekani, Trump pia alisema "tunatuma armada ambayo ina nguvu zaidi. Pia tunazo nyambizi ambazo pia zina nguvu zaidi ya meli ya kubeba ndege."
Mapema wiki hii, kundi la Carl Vinson, ambayo inajumuisha meli ya kubeba ndege na meli nyingine ya kivita, zilibadilishwa njia kutoka Singapore hadi magharibi mwa bahari la Pacific ambapo ilifanya mazoezi na jeshi la mabaharia la Korea kusini.
Jeshi la mabaharia la Japan pia limepanga mazoezi ya kijeshi na meli za kivita za marekani, shirika la habari la Reuters lilisema.
Korea kusini imeongeza kufanya majaribio ya makombora miezi ya hivi karibuni, japokuwa imekatazwa na umoja wa mataifa dhidi ya matumizi ya nuklia na makombora.
0 Post a Comment:
Post a Comment