Putin: Uhusiano na Marekani chini ya Trump ni mbaya

 

Vladimir PutinHaki miliki ya picha 
Image caption 

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema kuwa uhusiano na Marekani umedhoofika zaidi tangu Rais Donald Trump aingie madarakani mwezi Januari.
Aliiambia runinga moja ya Urusi kuwa imani kati ya nchi hizo mbili imepunguka.
Matamsdhi hayo yalitolewa wakati waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Urusi alikutana na mwenzake wa Marekani mjini Moscow, wakati pia kuna msukosuko kuhushu shambulizi linalokisiwa kuwa la kemikali nchini Syria.
Marekani imekuwa ikiitaka Urusi kuacha kuiunga mkono serikali ya Syria.
Lakini Urusi imepinga mashambulizi ya angani yaliyofanywa na Marekani dhdi ya kituo cha wanahewa nchini Syria, kujibu shambulizi la serikali dhidi ya waasi katika mkoa wa Idlib.
Taarifa hiyo ilikuja wakati waziri wa mashauri ya ni za kigeni wa Marekani Rex Tillerson, alikuwa akifanya mazungumzo na waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Urusi Sergei Lavrov.
Kabla ya mkutano wa Moscow bwana Lavrov alisema kwa Urusi ilikuwa na maswali mengi ya kuuliza kuhusu yale yanayotoa Marekani.
Mashambulizi ya Marekani yamezua utata kuhusu sera za Marekani nchini Syria, huku baadhi ya maafisa wakitaka hatua kali kuchukuliwa dhidi ya Rais Assad.

Shambulizi eneo la Khan Sheikhoun lilisababisha vifo vya watu 89Haki miliki ya pichaEPA
Image captionShambulizi eneo la Khan Sheikhoun lilisababisha vifo vya watu 89
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: