Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo mchana mara baada ya kupokea taarifa ya maandalizi na kukagua Uwanja wa Jamhuri ambapo sherehe hizo zitafanyika na uwanja wa Nyerere Square ambako zitafanyika burudani mbalimbali kama sehemu ya maadhimisho hayo.
“Nilikuja kuangalia maandalizi ya sherehe hizo yamefikia wapi, najua kutakuwa na maonyesho ya kijeshi zikiwemo michezo na burudani kutoka Tanzania Bara za Visiwani,” amesema.
Majaliwa alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wakazi kutoka wilaya zote za Mkoa wa Dodoma na mikoa ya jirani wafike kwenye maadhimisho hayo ambayo kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania yanafanyika mkoani humo.
0 Post a Comment:
Post a Comment