Somo: TAFSIRI SAHIHI YA NENO "USIHUKUMU"

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM=>


Mhubiri:Bishop Zachary Kakobe
Kanisa:Full Gospel Bible Fellowship Dar es   salaam
Writer:Zachary John Bequeker

Watu wengi wenye dhambi hujificha katika kichaka cha neno "usihukumu" pale tunapoyataja makosa yao na dhambi zao na tunapowaeleza kwamba wataangamia kutokana na dhambi hizo hukimbilia neno "usihukumu" ili waendelee kutenda dhambi na asiwepo wa kuwakalipia,
Maandiko hayatafsiriwi kama apendavyo mtu fulani,(2petro 1:20, 3:16), iko tafsiri sahihi katika maandiko kwa kuyachunguza maandiko na kuyathibitisha kwa mashaidi wawili au watatu.
Watu hawa ambao wanakimbilia neno "usihukumu" wanalenga kuendelea kufanya dhambi na hawataki kuonywa au kukalipiwa katika ukengeufu wao, na wanatumia maandiko katika kuhalalisha yale wanayokuwa wameyalenga, iko mistari kadhaa wannayotumia kama ifuatavyo๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡
a/ (Yohana 3:17)
b/(Yohana 12:47)
c/(warumi 14:1-4)
Wanadai mtumishi mmoja wa Mungu hatakiwi kumkemea mtumishi mwingine mwenye imani potofu
d/(Mathayo 7:1-5)
๐Ÿ‘†๐Ÿ‘† hayo ndio maandiko wanayotumia watu ili kuwanyamazisha watu wanaowaonya.
Sasa twende kwenye tafsiri sahihi ya maandiko
๐Ÿ‘‰(Yohana 9 :39)
Yesu mwenyewe anasema amekuja kwa ajili ya hukumu ni kama vile inakinzana na maandiko hayo tuliyoorodhesha hapo juu, Mungu hajipingi, neno lake limehakikishwa mara 7, na pale tunapoona neno linakinzana ni sisi tumeshindwa kuyatafsiri maandiko vile inavyotakiwa
๐Ÿ‘‰Maandiko yanaposema usihukumu ni Yesu anatufundisha tufanye hukumu iliyo ya haki
(Yohana 7:24),
๐Ÿ‘‰(Warumi 14:1-4), andiko hili liliandikwa na Paulo kwa uvuvio wa Roho mtakatifu kwamba usimuhukumu mtumishi wa mwingine lakini yeye alimkemea Petro mbele ya wote kwa sababu alistahiri hukumu,(Wagalatia 2:11-14) hakumwita chumbani , ni mbele ya wote.
Huu ni uthibitisho waziwazi kwamba andiko hilo halina maana hiyo inayotumiwa na wengi wa hao wanaojitetea kwamba wasihukumiwe

Paulo mwenyewe anatufundisha kanisa kwamba sisi kama kanisa tunatakiwa tuhukumu,(1korintho 5:9-15) watu waliokengeuka tunatakiwa tuwatenge,
Baada ya kuona mifano ya maandiko hayo ambayo yanatuagiza tuhukumu sasa
twende kwenye tafsiri sahihi ya maandiko ambayo yanatumiwa kwa kupotoshwa na hao watu wanaotaka kujikinga katika uovu wao

a/(Yohana 3:17) Maneno haya yalikuwa yanazungumzia hukumu ya mwisho ambayo Yesu atahukumu ulimwengu, wakati huu wa torati hukumu ilikuwa inatolewa papo kwa hapo, yani mtu akiiba atakatwa mkono, akifumaniwa anazini atapigwa kwa maww mpaka kufa, n.k, kwa hiyo alimaanisha kuwa katika kipindi cha Yesu baada ya yeye kuja duniani hukumu ya namna hiyo haitakuwapo(Yohana 5:22)(2Tim 4:1) (Ufuno 20:11-)
Anaposema sikuja ulimwenguni kwa hukumu anamaanisha sikuja kuwatenga kondoo na mbuzi (Mathayo 25:41) bali amekuja kuokoa kila kiilichopotea.
Kuokoa maana yake ni kuwaeleza watu habari za Yesu na watubu ili wakwepe hukumu ya mwisho
Tunapowahubirii watu kwa habari ya toba na ondoleo la dhambi  tunawahukumu (Luka 24:47-49) na kila muhubiri ndanii yake amejaa nguvu ya Roho Mtakatifu (Yohana 9::39-41)
(Mika 3:8) (Yohana 12:47-48)
Inapotajwa kwamba Yesu hakuja kuhukumu ina maana kwamba hakuja kwa ajili ya hukumu ya mwisho, na pale anaposema amekuja kuhukumu ni pale anapohubiri neno juu ya makosa ya watu hao
(Isaya 58:1)
Sisi nasi lazima tuwahubiri watu makosa yao, kweli ya injili ya biblia lazima iambatane na toba, tusiwasikie watu ambao wanasema tusiwahukumu pale tunapoyataja makosa yao, tuonye tukalipie, tukemee juu ya maangamizo yanayokuja kwao (2Tim 4:1-2),
Tuwaambie kama Yesu alivyokuja kwa hukumu nasi tunakuja kwa hukumu juu yao, tumetumwa kuwahubiria makosa na dhambi zao.
 Kama wewe ni mchungaji dhambi haitakiwi kulelewa kanisani bali ikemewe hadharani ili wengine waogope (1Tim 5:20) (Tito 2:15)
Tusiogope kuwaonya watu wala kuwakalipia wenye dhambi lazima waonywe kwamba njia wanayoiendea si sawasawa, na tukimuonya mtu mara ya kwanza, na mara ya pili na ya tatu lakini anadumu kutenda dhambi huyo tunamkataa(yaan tunamtimua)(Tito 3:10-11)
(Yoshua 1:7), kwenda kushoto au kulia ni kukengeuka na kuiacha njia na mtu akitoka kwenye mstari(akikengeuka) huyo tusiache kumkalipia
(Waefeso 5:11) Tukiyakemea matendo ya giza hapo tunafanya mapenzi ya Mungu.

Tuje kwenye lile andiko ambalo linatumika zaidi na watu hawa๐Ÿ‘‰ (Mathayo 7:1-5)๐Ÿ‘ˆ kwamba tusihukumu tusije tukahukumiwa
Maana yake ni kwamba hatuwez kuwaambia watu juu ya makosa yao kama sisi tunafanya yaleyale. Sura hii ya 7 katika kitabu cha Mathayo ni muendelezo wa sura ya 6 ambayo Yesu alikuwa anashughurika na mafarisayo wanafiki ambao wanaonesha watu vidole wakati wao wanafanya yaleyale, walikuwa wanaona vibanzi katika macho ya wengine wakati wao wana boriti(kipande cha mbao) machoni mwao
Mfano (Mathayo 6:5)(Warumi 2:1-3) .Maana yake ni kwamba ni lazima uhakikishe unatubu dhambi zako kwa kumaanisha kuzihacha na kukaa katika mapenzi ya Mungu na hapo unakuwa na haki ya kuhubiri wengine makosa yao, mfano mtu amemwacha mke wake amemuoa mwingine lakini wewe hujaoa mke mwingine kama yeye hivyo una haki ya kumwambia juu ya makosa yake na hapo unakuwa hujahukumu kama wanavyosema wao. Kwa hiyo kama upo katika njia iliyo sahihi usiache kukemea uovu kwa ambao wamekengeuka, au wewe sio muasi una haki ya kumkemea aliye asi na ukifanya hivyo hiyo inaitwa hukumu iliyo ya haki
(Zaburi 50:16)(Rumi 2:21-24)
Asiye haki ndiye ambae haruhusiwi kuhubiri injili.
Kwa hiyo andiko hili haliwazuii watu ambao wako mbali na dhambi kuyakemea matendo ya giza, bali inawapa uhalali wa kuwakemea wenye dhambi kwa sababu wao wako mbali na dhambi zao

๐Ÿ‘‰(Warumi 14:1-4)
Tusidanganyike na watu wanaokuja na mafunuo,ufunuo ulio kinyume na mapenzi ya Mungu tuukatae na ufunuo unapaswa kuwa ufunuo wa roho (1korintho 12:7) , na ufunuo huo unatwaa yaliyo ya Kristo ambaye anajulikana kama neno la Mungu na kutupasha habari.(yohana 16:13-14)
Ukiwa mshirika wa kanisa hili la Fgbf unatakiwa ujae hukumu(uwe nuru ya ulimwenguni) ukiona kuna mahari wanapotosha neno la Mungu pigiza, usibabaishwe na nyuso za mitume wanaosema wana upako.
Kemea  sema,"wewe nabii uchwara njia uiendayo ni ya upotevu na hukumu inakusubiri" akisema "mbona unanihukumu" waambie Paulo alimkemea Petro kwa sababu alistahiri hukumu.
Nasi tunamfuata Paulo kama Tunavyomfuata Kristo.
Hatupaswi kusema tusimzungumze mtumishi fulani eti kwa sababu Mungu atashughurika naye, Mungu alitutuma sote twende ulimwenguni kote kuhubiri, wako wengine waliowekwa waalimu wengine wachungaji, tukemee uovu bila kusita.
Na kwa sababu hiyo tupige simu katika maradio pale ambapo kuna mada za neno la Mungu tuwaambie watu kweli, kwenye mada zote ambapo neno linapindishwa twende huko tukatoe hukumu ya haki.

๐Ÿ‘‰(Warumi 14:1-14)
Hapa haizungumzii juu ya dhambi,bali udhaifu wa imani,neno linasema tunakula vyote vinavyouzwa sokoni, lakini mtu mwingine akawa hali vyote, tusimuambie kwamba hajaokoka, au mwingine yeye akiumwa huwa anakemea tu homa inaondoka, tusiwanyooshee kidole wale ambao wanaenda hospitali na kuwaona hawajaokoka basi aliye dhaifu wa imani tumkaribishe tusimpe hivyo ambavyo hataki
๐Ÿ‘‰Habari ya kukemea mtumishi juu ya uovu iko palepale
Ikiwa umeokoka uwe jasiri wa kukemea dhambi
Mtumishi au mtu yeyote akikengeuka tumkemee na kumkalipia bila kusitasita tena hadharani ili wengine waogope.
•Tuma mahubiri WhatsApp kwa 0625966236
Kwa masomo  zaidi bonyeza link hii www.zakacheka injili.blogspot.com
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: