Waziri wa nchi anayeshughulia masuala ya Muungano na Mazingira January Makamba amesema kuwa changamoto za Muungano wa iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar zimetatuliwa kwa kiasi kikubwa kutoka 15 mwaka 2006 hadi kufikia changamoto tatu mwaka huu.
Tanzania itaadhimisha miaka 53 ya Muungano, wa nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar, wiki ijayo.
Waziri Makamba amezungumza hayo leo Mjini Dodoma alipokuwa katika mkutano na waandishi wa habari.
Mhe. Makamba amezitaja changamoto zilizobakia kuwa ni pamoja na usajili wa vyombo vya moto unaorahisisha kusafirisha magari kutoka Zanzibar kwenda Bara na kutoka Bara kwenda Zanzibar na kusema kuwa swala hili linafanyiwa kazi kwa kumalizwa kwa taratibu za kisheria.
0 Post a Comment:
Post a Comment