Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo amekutana na mabalozi wa Tanzania wanaoenda kuiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali.
Nia ya kukutana nao ni kujadili na kuhakikisha wanaimarisha uhusiano na kujenga urafiki kwenye nchi wanazowakilisha kwa lengo la kuitangaza Tanzania kiuchumi.
Waziri Mkuu aliwaaga mabalozi hao huku akiwataka kuwakutanisha watanzania waishio nje ya nchi kukutana na kufanya mikutano mara kwa mara.
Mabalozi hao ni wa nchi za Qatar, Ubelgiji, Afrika Kusini, Ujerumani,Comoro, Algeria, India na Sudan.
0 Post a Comment:
Post a Comment