Mawaziri wa mambo ya nje G7 waendelea na mkutano

Mawaziri wa mambo ya nje G7 waendelea na mkutano

  •  
Mkutano huo ni wa siku mbili ukijadili zaidi hali ya usalama wa dunia
Image captionMkutano huo ni wa siku mbili ukijadili zaidi hali ya usalama wa dunia
Mawaziri wa mambo ya nje wa kundi la nchi saba zinazoendelea kiviwanda maarufu kama G7, wako kwenye mjadala wa hatua inayofuatia kuhusu mzozo wa Syria, baada ya tukio la shambulizi la bomu lenye kemikali za sumu lililotekelezwa na vikosi vya serikali ya nchi hiyo.
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani, Rex Tillerson ametamka kwamba Washington itawawajibisha wote ambao walishiriki katika mashambulizi ya watu wasio na hatia mahali popote duniani .
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Boris Johnson amesema kwamba mkutano huo wa siku mbili unaofanyika nchini Italia kwenye mji wa Lucca utazingatia pia vikwazo zaidi dhidi ya viongozi wa jeshi la Urusi na Syria.
Ikulu ya Kremlin imesema inaweza kulipiza kisasi kwa Marekani kwa kitendo chake cha kuishambulia Syria kwa njia ya anga na hii imeionesha Washington kuwa haikuwa na nia ya kuonesha ushirikiano.
Na kusema kwamba hakuna mpango wowote kwa bwana Tillerson kukutana na Rais Putin wakati atakapokuwa kwenye ziara ya kiserikali mjini Moscow baadaye wiki hii.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: