THURSDAY, APRIL 6, 2017
MNH yaanza matibabu ya kuondoa uvimbe bila kupasua
Dar es Salaam. Hospitali ya Taifa Muhimbili leo imeanza kufanya matibabu ya kuondoa uvimbe 'fibroid' kwa wanawake bila kupasua ambao hufanyika kwa njia ya matundu madogo (laparoscopic Surgery).
Upasuaji huo uliofanyika leo katika chumba kikuu cha upasuaji, unaenda sambamba na mafunzo kwa vitendo kwa madaktari zaidi ya 30 ambao wanafuatilia moja kwa moja kwa njia ya luninga wakiwa chumba cha mkutano.
Akizungumza wakati wa upasuaji huo, Daktari Bingwa wa uzazi na magonjwa ya wanawake Vicent Tarimo alisema upasuaji wa aina hiyo kwa njia ya kawaida huchukua takribani saa moja na nusu mpaka mawili, lakini kwa njia hiyo ya kisasa wamefanikiwa kumtibu mwanamke aliyekuwa na uvimbe kwenye mirija ya uzazi kwa saa moja.
"Zaidi ya wanawake 15 watanufaika na upasuaji huu na wengi wamekuwa na tatizo la uvimbe sehemu mbalimbali kuzunguka kizazi," alisema.
0 Post a Comment:
Post a Comment