Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis amewasili nchini Misri kwa ziara fupi inayolenga kuimarisha uhusiano wa kidini na ulimwengu wa Kiislamu.
Ziara hiyo inajiri wakati ambapo kuna ongezeko la mauaji ya Wakristo waliopo katika mashariki ya kati hususan wale wa jamii ya kanisa la Coptic.
Mapema mwezi huu kundi la Islamic state lilikiri kutekeleza shambulio la mabomu ya makanisa mawili ya Coptic.
Papa Francis atakutana na rais wa Misri na kutoa hotuba kuhusu amani katika chuo kikuu cha Al-Azhar, taasisi ya masomo ya Kiislamu miongoni mwa madheheu ya Sunni.
Ataonyesha umoja wake na mwenzake wa kanisa hilo Tawadrod II akijumuika naye katika kanisa lililoshambuliwa mnamo mwezi Disemba.
Uhusiano kati ya Vatican na Waislamu wengi ulishuka 2006 wakati mtangulizi wa Papa Francis Benedict alipoonekana akihusisha Uislamu na ghasia.
0 Post a Comment:
Post a Comment