Wizara ya Ulinzi nchini Marekani imesema kuwa inamchunguza aliyekuwa mshauri wa maswala ya usalama wa rais Donald Trump kuhusu malipo aliyopokea kutoka kwa kampuni zinazohusishwa na serikali ya Urusi.
Michael Flynn aliondoka katika serikali ya Trump baada ya siku 24 pekee afisini baada ya kubainika kwamba alimdanganya makamu wa rais kuhusu mawasiliano yake na balozi wa Urusi.
Wachunguzi wa bunge la Congress wanasema kuwa wakati jenerali Flynn alipoondoka katika jeshi alionywa kutochukua malipo yoyote ya serikali ya kigeni bila ruhusa.
Msemaji wa ikulu ya Whitehouse Sean Spicer alisema kuwa ilikuwa sawa kwa inspekta janerali huyo wa idara ya ulinzi ya Pentagon kuchunguza madai ya kufanya makosa.
0 Post a Comment:
Post a Comment