Papa Francis ataongoza misa ya Wakatoliki nchini Misri hii leo katika siku ya pili na ya mwisho ya ziara yake ya Cairo.
Ibada hiyo itafanyika katika uwanja wa wanajeshi, na itaongozwa kwa lugha ya Kiarabu na Kilatino.
Anatarajiwa kurejelea ujumbe wake wa jana ambapo aliwarai viongozi wa dini zote kukemea uhalifu wowote unaotekelezwa kwa misingi ya kidini.
Jana Papa Francis alizuru kanisa moja mjini Cairo Misri ambapo takriban Wakristo 30 waliuawa katika shambulio lililotekelezwa na wapiganaji wa Islamic State mwezi Disemba mwaka jana.
Aliandamana na kiongozi wa kanisa la Coptic nchini humo, Pope Tawadros.
0 Post a Comment:
Post a Comment