Rais wa Marekani Donald Trump amekuwa rais wa kwanza wa taifa hilo kuhutubia muungano wa wanaharakati wa uhuru wa kumiliki bunduki, NRA, baada ya kipindi cha zaidi ya miaka 30.
Akiongea hapo jana, mkesha wa siku zake mia moja madarakani, rais Trump ameahidi kuunga mkono na kulinda haki ya umiliki wa bunduki.
Huku mamia ya wanaharakati hao wakishangilia, rais Trump amewaahidi kwamba atakuwa mshirika wao mkuu katika ikulu ya White house.
Bwana Trump amesifu mafanikio yake uongozini katika kipindi cha siku 100 za kwanza kwa kusema kwamba ametekeleza mengi.
Hapo jana, rais Trump alitia saini agizo la urais ambalo huenda likapisha uchimbaji wa mafuta na gesi katika maeneo ya Arctic.
0 Post a Comment:
Post a Comment