POLISI Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kikosi cha Usalama Barabarani, wamekusanya zaidi ya Sh milioni 888 kwa siku tano kutokana na makosa ya usalama barabarani.
Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Simon Sirro alisema ukamataji wa makosa hayo ulifanyika Aprili 19 hadi 23, mwaka huu.
Alisema magari yaliyokamatwa yalikuwa 9,401, pikipiki 1,169, na mengine ya binafsi na malori 19,022.
Alisema waendeshaji bodaboda 10 walifikishwa mahakamani kwa kutovaa helmet na kupakia ‘mishkaki’. “Kama kila mtu atazingatia sheria na matumizi sahihi ya barabara, ajali za barabarani zitapungua na hivyo kuepusha vifo na majeruhi vinavyosababishwa na ajali,” alisema Sirro.
like, comment and share
0 Post a Comment:
Post a Comment