Hatua hiyo inatokana na kuchelewa kukamilika kwa matengenezo ya mfumo wa upozaji injini mbili za kivuko hicho.
Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa) imesema matengenezo hayo yalianza jana saa 5:50 usiku na kukamilika leo saa 12:30 asubuhi.
“Ifahamike kuwa kivuko cha Mv Magogoni kinatoa huduma ya uvushaji abiria, magari na mizigo kwa saa 24 kila siku na kwa siku zote saba za wiki. Hivyo, uangalizi wa kivuko hicho ni muhimu kwa ajili ya usalama wa abiria na mali zao.
“Temesa inaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza kwa watumiaji wa kivuko na kuahidi kuwa huduma zake zitaboreka zaidi baada ya ujio wa kivuko kipya cha Mv. Kazi hivi karibuni kwa ajili ya kutoa huduma kati ya eneo la Magogoni na Kigamboni,” ilisema taarifa hiyo.
000
0 Post a Comment:
Post a Comment