UVCCM yatangaza safu mpya




 Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM) umetangaza safu yake mpya ya viongozi wa idara mbalimbali katika umoja huo.
Katibu Mkuu UVCCM, Shaka Hamdu Shaka amesema idara hizo ambazo awali zilikuwa nne sasa hivi zimeongezwa na kufikia tano.

Aliwataja waliopitishwa na idara zao kwenye mabano Jokate Mwegelo (Uhamasishaji na Chipukizi), Dorice Obed (Uchumi,Uwezeshaji na Fedha), Daniel Zenda(Idara ya Vyuo Vikuu), Mohamed Abdalla(Oganaizesheni, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa) na Israel Sostenes wa Idara ya Usalama na Maadili.

Katika hatua nyingine Shaka aliwataka vijana kote nchini kuendelea kulinda Muungano ambao Aprili 26 unatarajia kufikisha miaka 53 ya kuzaliwa kwake.
"Hii ni tunu kubwa kwa Taifa letu hivyo vijana tuna wajibu wa kuulinda na kufanya kila linalowezekana kuhakikisha amani na utulivu vinaendelea kutawala nchini,"amesema Shaka.

Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: