Uchaguzi mkuu Ufaransa 2017: Sifa na sera zao wanaowania urais


Haki miliki ya picha
Wagombea kumi na mmoja wanawania urais kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika mnamo Jumapili.
Kuna wawaniaji watano wanaopigiwa upatu kufanya vyema, lakini kuna uwezekano kwamba hakuna atakayepata ushindi katika duru ya kwanza.
Kuna uwezekano kwamba huenda kukawa na duru ya pili ya uchaguzi kati ya wagombea wawili watakaoongoza uchaguzi wa Jumapili.
Uchaguzi wa marudio unafaa kuanyika tarehe 7 Mei.
Kwa mara ya kwanza katika miaka 15, kuna uwezekano mkubwa kwa chama cha mrengo wa kulia cha National Front kinachoongozwa na Marine Le Pen kushinda.
Mwanasiasa wa mrengo wa kati Emmanuel Macron anaonekana kushindana naye katika kura za maoni.
Mwanasiasa wa Republican wa mrengo wa kati-kulia François Fillon ambaye zamani alitarajiwa kufanya vyema, bado anawania licha ya kwamba anachunguzwa kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za umma.
Mgombea wa mrengo wa kushoto Jean-Luc Mélenchon, pia ana uungwaji mkono mkubwa.
kwa mara ya kwanza katika historia ya Ufaransa karibu, rais anayeondoka kutoka chama cha Kisoshialisti François Hollande hawanii muhula wa pili kutokana na kushuka kwa umaarufu wake.

Marine Le Pen, National Front (FN)

Haki miliki ya picha
Alichukua uongozi wa chama cha FN kutoka kwa babake Januari 2011 na alimaliza wa tatu uchaguzi wa urais mwaka uliofuata.
Alisaidia chama hicho kupata mafanikio makubwa uchaguzi wa majimbo mwishoni mwa 2015.
Kura za maoni zinaonesha anashindana vikali na Emmanuel Macron lakini kuna uwezekano huenda asimshinde kwenye duru ya pili.
Marine Le Pen, 48, ni mwanasheria na aliwahi kuongoza kitengo cha sheria katika chama cha FN.
Alichaguliwa kuwa mbunge katika Bunge la Ulaya 2004 ambapo aliwakilisha Kaskazini Magharibi mwa Ufaransa.
Amepewa talaka mara mbili na ana watoto watatu. Huishi viunga vya magharibi vya mji wa Paris.

Emmanuel Macron, En Marche (Tunasonga)
 Haki miliki ya pi
Ana miaka 39, na huenda akawa rais wa Ufaransa mwenye umri mdogo zaidi.
Kura za maoni zinaonesha kwamba huenda akaingia kwenye uchaguzi wa duru ya pili Mei 7 na kwamba akifanikiwa na iwe kwamba anashindana na Marine Le Pen, basi atamshinda.
Yeye si mbunge na hajawahi kuwania wadhifa wa siasa awali.
Alikuwa mwanafunzi mwerevu na amefanikiwa sana kama mwanabenki anayehusika katika uwekezaji.
Emmanuel Macron alihudumu kama mshauri wa kiuchumi wa Rais Hollande kabla ya kuteuliwa waziri wa uchumi mwaka 2014.
Macron ni mumewe mwalimu wa zamani wa Kifaransa Brigitte Trogneux ambaye ni mkubwa wake kwa umri kwa miaka 20.

François Fillon, Republican

Haki miliki ya picha
Bw Fillon, 62, alipata uungwaji mkono sana alipotangaza kwamba angewania urais kupitia chama hicho cha mrengo wa kati-kulia.
Aliwashinda wanasiasa wawili, Nicolas Sarkozy na Alain Juppé, ambao walikuwa wamekumbwa na kashfa chungu nzima.
Bw Fillon naye sasa amekabiliwa na kashfa.
Bw Fillon alisomea sheria na mumewe anatoka Wales, Penelope Clarke. Walioana mwaka 1980 eneo la Llanover, karibu na Abergavenny.

Jean-Luc Mélenchon, La France Insoumise (Ufaransa haitetereki)
 Haki miliki ya picha
Wasoshialisti walipokuwa wanapoteza uungwaji mkono, mwanasiasa wa mrengo wa kushoto Jean-Luc Mélenchon, 65, aliamua kutumia fursa hiyo kujinadi.
Ni miongoni mwa wanaopigiwa upatu kufanya vyema.
Anaungwa mkono na chama cha Kikomunisti nchini humo.
Anasema mifumo ya uzalishaji, biashara na matumizi ya bidhaa na huduma lazima ibadilishwe.
Alikihama chama cha Kisoshialisti Novemba 2008 na akaanzisha chama cha Kushoto akiwa na Marc Dolez. Alijiunga na kundi la uchaguzi la Left Front na akachaguliwa mbunge wa Bunge la Ulaya 2009 ambapo ameendelea kuhudumu.

Benoît Hamon, Socialist (Wasoshialisti)
Haki miliki ya pich
Benoît Hamon alikuwa waziri wa elimu na ni mwasi wa mrengo wa kushoto ndani ya chama cha Kisoshialisti.
Alimshinda waziri mkuu wa zamani kwenye mchujo Manuel Valls.
Anafahamika kama Bernie Sanders wa ufaransa.
Bw Hamon, 49, anatatizika kupata uungwaji mkono kinyang'anyiro cha urais, sana kutokana na ushindani kutoka kwa Jean-Luc Mélenchon. Ametatizika pia kupata uungwaji mkono wa watu wote ndani ya chama cha Kisoshialisti ambacho kimegawanyika.
Anataka kuhalalisha bangi.
Mwanandoa wake ni Gabrielle Guallar na wana mabinti wawili.

Wagombea wengine ni kina nani?
Kuna wagombea wengine sita uchaguzi huu wa mwaka 2017.
Haki miliki ya
Nathalie Arthaud, Lutte Ouvrière (Workers' Struggle / Mapambano ya Wafanyakazi), 46, Trotskyist: anataka kupiga amrufuku watu kufutwa kazi na kampuni kupunguza nafasi za kazi, aongeze mishahara na malipo ya uzeeni hadi €1,800, awezeshe wafanyakazi kumiliki kampuni na wamiliki nyenzo za uzalishaji.
François Asselineau, Union Populaire Républicaine (Popular Republic Union), 59, Mwanataifa na mpinzani wa Marekani: anataka Ufaransa ijiondoe EU na Nato na iache kutumia sarafu ya euro. Aidha, ataifishe tena kampuni na mashirika makubwa.
Jacques Cheminade, 75, Mtumishi wa umma wa zamani anayetaka Ufaransa ijitoe EU na iache kutumia euro. Ni mfuasi wa Mmarekani anayeamini katika njama kubwa ya kuidhibiti duniaLyndon LaRouche.
Nicolas Dupont-Aignan, Debout La France (Stand Up France), 55, Mwanagaul: Anataka Ufaransa iache kutumia euro na EU ivunjwe. Anadai alipokea ujumbe mfupi kutoka kwa Fillon kumhimiza ajiondoe kwenye kinyang'anyiro.
Haki miliki ya picha
Jean Lassalle, 61, anafuata siasa za mrengo wa kati. Ni mbunge asiyeegemea chama chochote anayetaka mikataba kuhusu Umoja wa Ulaya ijadiliwe upya. Alisusia chakula siku 39 mwaka 2006 kujaribu kupigania nafasi 140 za kazi katika kiwanda kimoja. Mwaka 2013 alitembea umbali wa kilomita 5,000.
Philippe Poutou, 50, New Anti-Capitalist Party - Ni mfanyakazi waFord na anataka umri wa kustaafu upunguzwe hadi miaka 60, saa za kufanya kazi zipunguzwe hadi 32 kwa wiki na huduma za utoaji mimba na uzazi wa mpango ziwe zikipatikana kwa urahisi. Wengi walimsifu alipowashambulia Fillon na Le Pen kwenye mdahalo wa runinga kuhusu tuhuma za ufisadi.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: