Makombora ya Korea Kaskazini
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelani vikali jaribio la hivi karibuni la makombora lililofanywa na Korea kaskazini.
Katika taarifa iliyotolewa na baraza hilo, limeelezea jaribio hilo, kama la ''kuvuruga amani'' baya na la kuuchokoza na kutojali Umoja wa Mataifa.
Baraza la Usalama linatarajiwa kukutana kujadili jaribio hilo la makombora lililofanywa siku ya Jumapili.
Korea Kaskazini imesema imefanikiwa kujaribu kombora lake la masafa ya kati, ambalo lilipaa karibu kilomita mia tano kabla ya kutua katika bahari ya Japan.
0 Post a Comment:
Post a Comment