Fahamu mengi kuhusu Rais Zuma

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM=>
Jacob Zuma ni Rais wa aina yake na mwenye utata kuwahi kutokea Afrika Kusini baada ya utawala wa weupe mwaka 1994. Amekuwa ni mwanasiasa mwenye maisha tisa akiponea chupuchup kashfa kadhaaa ambazo zineweza kuangamiza kabisha nafasi na historia ya kisiasa ya mtu mwingine yeyote.
Lakini Zuma aliyezaliwa katika familia masikini na baadae kusihi uhamishoni sababu ya kupinga ubaguzi wa rangi kabla ya kupanda ngazi na kushika hatamu kama rais wa watu, hawezi kunusurika kashfa hizi kila mara.
Muula wake wa pili na wa mwisho unafikia ukomo ,siyo kiongozi tena wa chama tawala ANC (African National Congress) licha ya kukana mara zote tuhuma za rushwa dhidi yake tuhuma hizo zimekuwa zikijirudia kila mara.
African National Congress (ANC) President Cyril Ramaphosa (L) celebrates the Congress" 106th anniversary celebrations with Kenyan President Uhuru Kenyatta (R) and president of South Africa Jacob Zuma, in East London, South Africa, January 13, 2018.Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionCyril Ramaphosa (kushoto) alichukua nafasi ya Mr Zuma kama kiongozi wa ANC
Itakuwa si jambo la busara kumfuta sasa wakati mapema kabla ya hata kuingia madarakani Zuma tayari alikuwa tayari anatuhuma kadhaa.
Urais wa Zuma ulitiliwa mashaka hata kabla ya kuingia madarakani, mwaka 2009 kueleke uchaguzi mkuu mwaka huo tayari zuma alikuwa akikabiliwa na tuhuma za rushwa na ubakaji.
South African President Jacob Zuma (L) sings and dances with his newlywed Tobeka Madiba (R) at their wedding ceremony on January 4, 2010 in a colourful Zulu traditional wedding outfit at Zuma's rural homestead of NkandlaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMr Zuma alisifika kwa uwezo wake wa kucheza
Alituhumiwa kumbaka rafiki wa familia yake ambaye anaishi na virusi vya ukimwi mwaka 2006, lakini licha ushaidi Zuma aliambia mahakama kuwa alioga ili kujikinga na kupata virusi vya ukimwi ambavyo vinge muandama muda wote wa uraisi wake.
Tuhuma za rushwa dhidi yake hazikupotea kirahisi hata baada ya kutupiliwa mbali kiutata na tume ya mwendesha mashtaka wa serikali juma moja kabla ya uchaguzi ulio muweka madarakani
Likoni tuhuma za utakatishaji wa fedha na kupanga mpango katika mkataba tata wa silaha wa mwaka 1999 bado zina muandama, kwani mwaka 2017 mahakama ya upeo nchini humo iliamua tuhuma 18 za rushwa zidi yake zita rejelewa
Mara zote Zuma amekanusha tuhuma hizo na kuapa kuachia ngazi ikithibitika kama ni kweli amehusika.
'Raisi wa Watu'
Ulikuwa ni utu wake ndio ulimpeleka Zuma madarakani mwaka 2009 wafuasi wake waliona namna alivyokuwa akikubalika na wengi na kushika hisia zao na kuwa mbadala wa Rais Thabo Mbeki ambaye alionekana kuwa mbali na watu.
''Ni mtu anayesikiliza, hajifanyi kuwa mungu mtu ''alisema mfuasi wake mmoja ambaye jina lake halikufahamika wakati Bw Mbeki alipokuwa anaelekea kuanguka huku wafuasi wake wakielezwa kuongoza mapambano ya kumuweka Zuma madarakani baada ya kunyakua uongozi wa chama ANC mwaka 2007.
Ukaribu wa bwana Zuma usimamizi na utetezi wa mila na desturi katika familia ni miongoni mwa sababu zilizo pelekea kujizolea wafuasi hasa kwa raia masikini wan chi hiyo wengi wao wakiwa ni wakaazi wa vijijini.
A view of the controversial homestead of South African President Jacob Zuma in Nkandla on January 21, 2014Haki miliki ya pichaAFP
Image captionNyumba ya Bw Zuma's huko Nkandla ilimletea changamoto chungu nzima ya kisiasa
Zuma mwenye miaka 75 anajivunia ndoa za mitara kama ilivyo ilivyo desturi ya wazulu Zuma kwa sasa ana wake wa nne ameoa mara sita ana watoto 21 na mmoja wa wake zake raia wa Msumbiji Kate Mantsho alijiua mwaka 2000.
Kadhalika anasifa ya kutokuwa mwaminifu katika ndoa zake na analea mtoto wa nje ya ndoa na mwanamke mwingine.
Imani hii ya Raia kwa Zuma kama rais wa watu haikudumu kwa muda mrefu ,mapema mwaka 2013 moshi ulianza kufuka baada ya Zuma kuboresha makazi yake ya kijijini kwao Nkandla kaskazini mwa KwaZulu-Natal akitumia hela za serikali.
Wakati wa ibada ya mazishi ya Rais wa kwanza mweusi wa Taifa hilo Nelson Mandela wafuasi wa ANC walikuwa wakimkosoa wazi wazi mbele ya wageni mbali mbali wa kimataifa akiwemo aliyekuwa Rais wa Marekani wakati huo Barrack Obama.
''Anakula wakati tuna njaa'' mmoja wa waandamanaji alisema na kuamsha hasira kwa waandamanaji juu wa maboresho zuma aliyofanya kwenye makazi yake huko Nkandla ikiwa na eneo la kufugia ng'ombe, ukumbi wa Sanaa , bwawa la kuogelea ,sehemu ya wageni na banda la kuku.
Bw Zuma alifanikiwa kulipa hela za ziada alizotumia.

Visa vya kisheria vinavyomuandama Zuma

President Jacob ZumaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
  • 2005: Alituhumiwa kwa rushwa yamabilioni ya dola kwenye mkataba wa silaha wa mwaka 1999 madai ambayo yalitupiliwa mbali kabla hajawa rais mwaka 2009
  • 2016: Mahakama iliamuru ashitakiwe kwa makosa 18 ya rushwa dhiya yam kata wa silaha ambao alikatia rufaa
  • 2005: Aishitakiwa kwa kumb'aka rafiki wa familia na kufutiwa mashitaka2006
  • 2016: Mahakama iliamuru kuwa amekiuka kiapo chake kama raisi na kutumia fedha za serikali kuboreshamakazi yake binafsi fedha ambazo alizilipa baadae
  • 2017: Wakili wa serikali alisema ateu jaji kiongozio wa kamati ya kuchunguza iwapo ana uhusiano na familia tajiri ya Gupta madai ambayo ameyakanusha
  • 2018: Zuma alikubali maombi hayo

Miaka mitatu Mahakama kuu nchi Afika kusini iliamua kwamba amekiuka katiba kwa kushindwa kulipa pesa za serikali alizo tumia kuboresha makazi yake binafsi
Rasi Zuma aliwaomba radhi raia wa nchi hiyo kwa tuhuma hizo na kulipa fedha hizo.
Lakini tuhuma hizi za makazi zilitarajiwa kufunikwa na tuhuma kubwa zaidi za namna alivyoingia madarakani.
Baada ya muda kidogo mahusiano ya Zuma na familia tajiri ya India Gupta yakaanza kumulikwa tuhuma zikiwa ni kwamba walishinikiza uteuzi wa baraza la mawaziri ili waweze kupata mikata yenye fedha nyingi ya serikali.
Tuhuma hizi zimepingwa vikali na Zuma mwenyewe na hata familia ya Gupta.
Akiwa na miaka 17 Zuma alijiunga na ANC na kuwa mwanacha hodari katika tawi lake la Jeshini Umkhonto We Sizwe, in 1962.

Wake zake Zuma

African Union chairperson Nkosazana Dlamini-Zuma arrives at the Elysee palace to participate in the Elysee summit for peace and safety in Africa on December 6, 2013, in ParisHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMs Dlamini-Zuma anaonekana kuwa mrithi wake Mr Zuma
  • Gertrude Sizakele Khumalo alimuoa mwaka 1973
  • Nompumelelo Ntuli (2008)
  • Thobeka Madiba (2010)
  • Gloria Bongi Ngema (2012)

Wake aliotalikiana nao

  • Nkosazana Dlamini-Zuma (alimuoa mwaka 1972; na kuachana naye 1998)
  • Kate Mantsho (alimuoa 1976; alifariki 2000)
Alihukumiwa kwa kula njama za kutaka kupindua serikali ya kibaguzi ya makaburu na kufungwa miaka 10 katika gereza la watu hatari zaidi katika kisiwa cha Robben pamoja na Nelson Mandela.
Inaelezwa Zuma alikuwa akichochoa morali ya wapigania uhuru hawa kwa nyimbo na tungo za kizalendo na wengi wana amini hiki ndo kilimfanya kuwa maarufu miongo ni mwa Raia hata wale wa vijini kabla ya kuupata uraisi
Chini ya utawala wa Zuma uchumi umekuwa ukiyumba na ididi ya idadi ya wasio kuwa na ajira imeongezeka kwa asilimia 28 huku kukiwa na maandamano ya mara kwa mara watu wakidai maisha bora.
Thousands of South African opposition Economic Freedom Fighter (EFF) supporters, march towards the constitutional court where judges heard a case over public money spent on President Jacob Zuma's private house on February 9, 2016 in JohannesburgHaki miliki ya pichaAFP
Image captionVyama vya upinzani walimpinga Jacob Zuma kupitia maandamano na mahakamani
Ni wazi kwamba yapo Zuma aliyoshinda kama Rais zuma ameshinda kukosolewa na harakati baada ya kutangaza sera ya Ukimwi ya taifa hilo mwaka 2010 na hili limepunguza kwa kiwango kikubwa vifo vya waathirika wa Ukimwi kwa kuwapatia dawa za kufubaza makali ya virusi hivyo ARV.
Afrika ya kusini ina wastani wa watu millioni tano wanaoishi na virusi vya ukimwi ikiwa ni kiwango cha juu kuliko taifa lolote.

Kuzomewa

Ni kweli kwamba Julius Malema na chama chake cha Economic Freedom Fighters (EFF) wamekuwa Yuma ya majaribio kadhaa ya kutaka kumtoa madarakani Rais Zuma
Kura ya tisa ya kutokuwa na iamani naye ilipigwa siku chache kabla ya kuhutubia taifa.
Kwa sasa Cyril Ramaphosa anafuata nyayo za Zuma wakati ambao kamati kuu ya chama imekuwa ikifanya vikao vya kutaka kumondoa madarakini zuma ili kujitenga na tuhuma za rushwa zinazo mkabili kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2019.
Ijapokuwa inaweza kuwa si busara kumfuta Zuma kwa sasa Zuma ambaye maana ya jina lake hilo la kizulu ni anaye tabasabu akiwatwanga maadui zake.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: