Tovuti rasmi ya rais wa Ukraine Petro Poroshenko imeshambuliwa na wahalifu wa mtandaoni kutoka Urusi, mamlaka yake imesema.
Imesema kuwa hatua hiyo inafuatia uamuzi wa rais huyo kupiga marufuku mitandao ya kijamii ya Urusi ambayo ni maarufu sana nchini Ukraine.
Kiev haikutoa ushahidi wowote unaohusisha Urusi na uvamizi huo.
Hatahivyo Urusi haijatoa tamko lolote kuhusu madai hayo ya Ukraine.
Utawala wa rais huyo wa Ukraine umesema kuwa hali hiyo 'imedhibitiwa' na hakuna tishio lolote katika kazi ya tovuti hiyo.
Saa kadhaa baada taarifa ya utawala huo, tovuti hiyo ilianza kufanya kazi kama kawaida huku viunganishi vyote vya habari katika ukurasa wa kwanza vikipatikana.
Uamuzi wa Ukraine kupiga marufuku mitandao hiyo ya Urusi mapema Jumanne ni mojwapo ya hatua ya kuiwekea vikwazo Urusi kwa kuiteka Crimea 2014 mbali na madai ya kuhusika na mzozo mashariki mwa Ukraine.
Mitandao iliolengwa ni pamoja na Vk.com na Odnoklassniki, Mtandao wa kutafuta, Yandex na huduma za barua pepe za Mail.ru.
Mtandao wa VK
Kampuni za huduma za mitandao zimeagizwa kufungilia mbali mitandao hiyo.
Mali zilizopo katika afisi za kampuni hizo nchini Ukraine pia zimepigwa tanji na kuwekewa vikwazo ijapokuwa haijulikani marufuku ya huduma hizo itatekelezwa vipi na iwapo Ukraine ina uwezo wa kuitekeleza.
Hatua hiyo ya rais ambayo ilipendekezwa na baraza la usalama la taifa hilo huenda ikawaathiri raia wengi wa taifa hilo kwa kuwa takriban raia milioni 14 wanatumia mtandao wa VK huku ule wa Odnoklassniki ukimaanisha waliosoma katika darasa moja ni maarufu.
0 Post a Comment:
Post a Comment