Tanesco yatoa tahadhari kwa wananchi


12 Mei 2017

Kaimu Mkurugenzi wa Tanesco nchini, Dk Tito
Kaimu Mkurugenzi wa Tanesco nchini, Dk Tito Mwinuka 
 Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limetoa tahadhari kwa wananchi likiwataka wasikae wala kufanya shughuli zozote karibu na miundombinu yake kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchi nzima.
Kaimu Mkurugenzi wa Tanesco nchini, Dk Tito Mwinuka amesema miundombinu ya umeme nchini kwa sasa inapata hitilafu za mara kwa mara hivyo wananchi wachukue tahadhari.
Dk Mwinuka amewataka wananchi kutoa taarifa mapema inapotokea hitilafu yoyote kwenye miundombinu ya umeme wakati mvua zinapoendelea kunyesha.
"Wasikae chini ya transfoma ya umeme… tunawaomba wananchi kutoa taarifa mapema maeneo yenye mafuriko au mkusanyiko wa maji mengi ili kusaidia kuchukua tahadhari," alisema Dk Mwinuka.

Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: