18 Oktoba 2017
Baada ya kimya kutawala kwa muda mrefu jijini Mwanza kwa kutokuwapo na mikutano ya kisiasa, kwa mara ya kwanza wanachama wa chama cha demokrasia na Maendeleo - CHADEMA walionekana wakiwa wamelipamba jiji la Mwanza kwa kuvalia sare zao za chama.
Zaidi ya wanachama 200 kutoka matawi 13 walikutana pamoja siku ya jana Jumanne wakiwa na magari sita aina ya coster, magari mawili madogo, bajaji na pikipiki iliyoongoza msafara huo kutoka kituo cha magari cha Tanganyika Mwanza mjini hadi kata ya Sangabuye-Igombe kwa msiba wa baba yake na mwanachama mwenzao wa tawi la dampo.
Wakiwa njiani vijana kwa wazee walikuwa wakinyosha vidole vyao juu na wengine walisikika wakisema PEOPLE'S - POWER.
Kiuhalisia wao hawakwenda kwa ajili ya maonyesho bali walienda kumfariji mwanachama mwenzao aliyekuwa amefiwa na baba yake. kwa sababu hiyo hawakuwa na kelele zozote wala fujo zozote.
Shughuli nyingi na kuu za msiba ziliendeshwa na chama, na hii inaonesha ni jinsi gani wanachama hawa walivyo na ushirikiano bila kujali ni mwanachama wa kawaida au ni kiongozi, kwa sababu hiyo watu wengi wakavutiwa na mfumo uliopo katika chama hicho.
=>Kwa sasa yamefikia matawi 21 ambayo yameshajiunga na mengine yakiwa mbioni kujiunga.
Utaratibu wa chama hiki ni endelevu, na ni ukweli usiopingika kuwa watu wengi wanavutiwa na mfumo huu, kwa sababu hiyo kila siku matawi huongezeka.
=> TUNDU LISSU KUTOKA HOSPITALI WIKI IJAYO
Tuma habari picha WhatsApp kwa 0625966236
=> TUFUATE FACEBOOK: zakacheka.blogspot.com na u-download APP yetu ya ZAKACHEKA huko
0 Post a Comment:
Post a Comment