Shughuli ya kurusha roketi huko Virginia Marekani ilisimamishwa dakika za mwisho baada ya ndege ndogo kuruka karibu na eneo shughuli hiyo ilikuwa ifanyika.
Roketi hiyo ya mizigo isiyo na burani ilitarajiwa kurushwa kwenda kituo cha kimataifa kilicho anga za juu (ISS) wakati shughuli hiyo ilisitishwa ghafla.
Walikuwa wameona ndege ndogo iliyokuwa ikiruka eneo lisiloruhusiwa umbali ya futi 500 katika kisiwa cha Wallops.
Urushaji wa roketi hiyo utaradiwa tena leo Jumapili.
Roketi hiyo imesheheni kilo 3,356 ya chakula, vifaa na bidhaa za sayansi kwa kituo cha ISS
Orbital ATK, iliyo na kandarasi ya dola bilioni 1.9 na shirika la anga za juu la Marekani Nasa kupeleka bidhaa katika kituo cha ISS ilipeperusha matangazo ya urushaji wa roketi hiyo.
0 Post a Comment:
Post a Comment