Miguel Diaz-Canel amekula kiapo rasmi cha uraisi kama raisi mteule wa Cuba huku akitaja vipaumbele vyake ikiwemo ahadi ya kuendelea na mfumo wa kanda wa kikomunisti wa chama kimoja.
Katika hotuba yake ya kwanza akiwa kiongozi wa taifa hilo, Diaz-Canel ambaye awali alikuwa makamu wa raisi alitangaza uaminifu wake kwa mapinduzi na kumsifu Rais anayemaliza muda wake, Raul Castro.
Nchi hiyo ilikuwa chini ya utawala wa miongo sita na bwana Castro na kakake Fidel ambaye alijiuzulu mnamo mwaka 2008.
Katika hotuba yake ndefu, Castro amesema kwamba atasalia kama kiongoiz mkuu wa chama cha kikomunisti na pia amiri jeshi mkuu na kiongozi wa majeshi.
Download App Yetu hapa chini, Bonyeza picha:-
0 Post a Comment:
Post a Comment