Kahawa hupunguza hatari ya kupatwa ya ugonjwa wa Ini na Mapafu

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM=>

Unywaji wa kahawa kiasi ni salama , na vikombe vitatu kwa siku vya kahawa vinaweza kuwa na faida kadhaa za kiafya , kulinga na utafiti uliofanywa na BMJ.
Utafiti huo ulibaini kuwa unywaji wa kiasi hicho cha kahawa unaweza kumfanya mnywaji kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya ini na saratani na kupunguza kiwango cha klupata kiharus - lakini watafiti hao wanasema hawawezi kuthibitisha kuwa kahawa ndio sababu ya upungufu wa athari hizo .
Unywaji wa kiwango kikubwa cha kahawa wakati wa ujauzito unaweza kuwa hata hatari , umethibitisha utafiti huo.
Wataalam wanasema hata hivyo kuwa watu hawapaswi kuanza kunywa kahawa kwa sababu za kiafya ama kama njia ya kuzuwia magonjwa.
Watafiti katika Chuo Kikuu cha Southampton walikusanya taarifa kuhusu athari za unywaji wa kahawa kwa binadamu kwa mwili wa binadamu kwa ujumla , wakizingatia tafiti zaidi ya 200 , ambazo nyingi kati yake zilikuwa za uchunguza.
Watafiti walipolinganisha watu wasio kunywa kahawa , na wale wanaokunywa takriban vikombe vitatu vya kahawa kwa siku walionekana kupunguza uwezekano wa kupata kiharusi.
Faida kubwa ya unywaji wa kahawa zilionekana katika kupunguza hatari ya ugonjwa wa ini, pamoja na saratani.
Tuma habari picha,video za matukio mbalimbali WhatsApp kwa 0625966236
Lakini Profesa Paul Roderick, mmoja wa waandishi wa utafiti huo kutoka kitivo cha tiba katika Chuo Kikuu cha Southampton, anasema utafiti huo haukusema ikiwa unywaji wa kiasi fulani wa kawaha ulileta ulikuwa na mabadiliko fulani.
"Masuala kama vile umri,ikiwa watu walikuwa ni wavutaji wa sigara au hapana na ikiwa walifanya mazoezi ya kimwili kwa kiasi fulani pia yalichangia katika athari za unywaji kahawa ," alisema.


Imagti huu unaunga mkono tafiti na uchunguzi wa hivi karibuni wa unywaji wa kahawa wa kiwango hicho

Watafiti wanasema kuwa wanywaji wa kahawa wanapaswa kunywa kinywaji hicho "kwa kuzingatia afya " - ikiwa ni pamoja na kuepuka matumizi ya sukari nyingi, maziwa au kunywa na vitafunio vyenye mafuta.
Na wanatoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi zaidi wa kimatibabu ya juu ya unywaji wa kahawa ili kubaini zaidi faida za kiafya zinazoweza kutokana na unywaji wa kahawa.
Tuma habari picha,video za matukio mbalimbali WhatsApp kwa 0625966236
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: