Kenya:Reli mpya ya kisasa SGR yazinduliwa


31 Mei 2017

Reli mpya ya SGR yazinduliwa Kenya
Reli mpya ya SGR iliozinduliwa na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
Kenya imezindua reli mpya kati ya mji wa Mombasa hadi Nairobi ikiwa ni miezi 18 mapema.
Reli hiyo iliotengezwa kupitia ufadhili wa shilingi bilioni 3.2 kutoka serikali ya China ndio mradi mkubwa wa miundo msingi kuwahi kutekelezwa na serikali tangu taifa hilo lijipatie uhuru wake.
Mradi huo umechukua takriban miaka mitatu na nusu kwa kutumia teknolojia ya ujenzi wa reli ya China kukamilika.
Reli hiyo inatarajiwa kuunganisha Sudan Kusini, DR Congo ,Burundi na Mombasa.
Ni reli ya kwanza katika kipindi cha karne moja.
Safari ya kutoka Mombasa kuelekea Nairobi na treni ya kisasa itachukua saa nne na nusu ikilinganishwa na saa tisa kwa kutumia basi na saa 12 kwa kutumia treni ya zamani.
Nauli ya watu watakaokalia viti vya kawaida ni shilingi 900 huku wale watakaosafiri kwa kutumia business class wakilipa shilingi 3,000.
Rais Uhuru Kenyatta alisema wakati wa uzinduzi wa reli hiyo ambayo imeanzishwa mwamko mpya katika historia ya Kenya.
''Historia ilianzwa miaka122 iliopita wakati Waingereza waliokuwa wametawala taifa hili walipoanzisha treni hiyo iliokuwa haijulikani inakokwenda na kupewa jina Lunatic Express
''Leo licha ya kukosolewa pakubwa tunasherehekea Madaraka Express {ikitajwa baada ya siku ambayo Wakenya walijipatia uhuru wao kikamilifu} badala ya Lunatic Express.
Gharama ya mradi huo imekosolewa na upinzani ambao unasema mradi huo umeigharimu Kenya fedha nyingi mno.
Vilevile wamemshutumu rais Kenyatta kwa kuomba fedha kutoka China bila mpango.
Serikali nayo inasema kuwa ni sharti iwekeze katika miundo msingi ili kuvutia wawekezaji.

Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: