RC Makonda awavaa vigogo wanaopinga kampeni yake



Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema wale wote wanaosema kampeni yake ya kuwasaidia akina mama waliotelekezwa na watoto imevunja sheria, pengine wana watoto nje na wanaogopa kujitokeza.

Makonda ameyasema hayo Aprili 19, katika uzinduzi wa hospitali ya kisasa ya mama na mtoto iliyopo Chanika iliyojengwa kwa msaada wa Shirika Maendeleo la Kimataida la Korea (Koica).

“Eti wanasema navunja sheria, natakiwa nifanye faragha kama unataka faragha tunza mtoto. Mimi siogopi, nipo tayari kufungwa lakini kwa ajili wa kutetea haki za watoto. Pengine hao wanaosema navunja sheria wana watoto wao nje wanaogopa kujitokeza,” amesema.

Jana, Aprili 18 Waziri wa Sheria na Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi  akiwa bungeni alisema kampeni hiyo inaweza kuleta hali ya sintofahamu na akabainisha kuwa inapaswa kufanyika faragha na sio kama inavyofanyika sasa.

Awali, Waziri wa Afya, Jinsia, Wanawake na Watoto,  Ummy Mwalimu alisema kampeni hiyo ni sahihi ila kasoro yake ni kutokuwa na faragha, lakini akasema kwa sasa inafanyika huku picha za watoto zikifichwa.

Aliyeibua hilo bungeni Aprili 18 alikuwa ni mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga aliyehoji uhalali wa kampeni hiyo na akahoji kama haivunji sheria na kuwavunjia haki wanawake na watoto.

Download App Yetu hapa chini, Bonyeza picha:-



Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: