Wafanyakazi wa serikali kutovaa Niqab Ujerumani


  • 28 Aprili 2017
Vazi la Niqab kupigwa marufuku Ujerumani
Vazi la Niqab kupigwa marufuku Ujerumani
Bunge nchini Ujerumani limepiga kura ya kuunga mkono wafanyikazi wa serikali kutovaa vazi la kiislamu linaloficha uso la Niqab wakati wanapokuwa kazini.
Mswada huo sasa utapelekwa katika bunge kuu ili kuidhinishwa. Waziri wa maswala ya ndani Thomas de Maiziere alisema kuwa hatua hiyo imeweka wazi viwango vya uvumilivu miongoni jamii nyengine nchini humo.
Mnamo mwezi Disemba ,chansela wa Ujerumani Angela Merkel alitoa wito wa kupigwa marufuku kwa vazi hilo linalofunika uso linalovaliwa na wanawake kadhaa wa Kiislamu.
Vyama vya mrengo wa kulia vimekuwa vikishinikiza kupigwa marufuku katika maeneo ya umma kama vile nchini Ufaransa.
Zaidi ya wahamiaji milioni moja ,wengi wao wakiwa waislamui kutoka mashariki ya kati wamewasili nchini Ujerumani katika kipindi cha miaka miwili iliopita.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: