KUNGURU MWEREVU




>Siku moja yenye jua kali kunguru mwenye kiu alizunguka kila mahali akitafuta maji.

Alizunguka kwa muda mrefu lakini hakufanikiwa kupata maji yoyote . 

Ghafla, aliona jagi la maji chini ya mti. Alipaa kuelekea chini kuona kama kulikuwa na maji ndani ya jagi. Ndiyo, aliweza kuona maji ndani ya jagi! Kunguru alijaribu kusukumiza kichwa chake ndani ya jagi . 

Huzuni, alikuta shingo ya jagi ilikuwa ni nyembamba mno. "Nitafanya nini? Ninakiu kweli . Nitawezaje kunywa maji haya?" alisema. KIsha alijaribu kulisukuma jagi kwa kuliinamisha ili maji yamwagike lakini jagi lilikuwa ni zito mno.

 Aliangaza mahali na kuona mawe laini madogomadogo ya duara. Ghafla akapata wazo. Alianza kuyadonoa mawe moja baada ya jingine akiyadondoshea kwenye jagi. Punde si punde mawe yalijaa kwenye jagi . 

Kimo cha maji kiliongezeka . Hivi punde maji yakawa yanatosha kwa kunguru kunywa. Mpango wake ulifanikiwa.

       SOMO: UTAPATA SULUHISHO LA TATIZO LAKO KWA KUFIKIRI NA KUJIBIDIISHA SANA!!!

Imeandikwa na Zachary John Bequeker +255625966236 WhatsApp
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: