Marekani: Tuko tayari kwa mazungumzo na Korea Kaskazini

  • 28 Aprili 2017

Rex Tillerson (kulia) na balozi wa Marekani kwenye UN Nikki Haley, wakiwa kwenye mkutano
Rex Tillerson (kulia) na balozi wa Marekani kwenye UN Nikki Haley, wakiwa kwenye mkutano
Marekani iko tayari kwa mazungumzo na Korea Kaskazini yenye lengo la kuondoa zana za nuklia kutoka eneo hilo, kwa mujibu wa waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani.
Lakini amesema kuwa Marekani itatumia nguvu za kijeshi ikiwa itahitajika.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa China, mshirika mkubwa wa Korea Kaskazini, anasema makubaliano ya amani ndio njia pekee.
Bwana Tillerson aliliambia baraza la ulinza la Umoja wa Mataifa kuwa tisho la Korea Kaskazini la kushambulia majirani zake na zana za nuklia.
Maelfu ya wanajeshi wa Marekani wako nchi majirani wa Korea Kaskazini ikiwemo Korea Kusini na Japan.
Tillerson amezitaka nchi wachama wa Umoja wa Mataifa kuiwekea Korea Kaskazini vikwazo na kupunguza uhusiano wao wa kidiplomasia na nchi hiyo.
"Kwa miaka kadha Korea Kaskazini imekuwa ikiendesha kwa nguvu mpango huu hatari."
"Ni wakati wetu kuchukua hatua na kudhibiti hali," Tisho la Korea Kaskazini la kufanya shambulizi la nuklia dhidi ya Korea Kusini au Japan ni la kuwezekana, na ni muda tu kabla ya Korea Kaskazini kufanikiwa kupata uwezo wa kushambulia Marekani." alisema Tillerson.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: