Matumizi ya dawa za kuzuia magonjwa yanaweza kusababisha saratani ya utumbo
Matumizi ya dawa za kuzuia magonjwa, au 'antibiotic, kwa muda mrefu inaweza kusababisha uvimbe kwenye umbo ambao waweza kusababisha saratani.
Lakini wataalam wanasema kuwa utafiti zaidi lazima ufanywe ili kutoa ushahidi zaidi, na hivyo watu wasikome kutumia dawa hizi.
Asilimia 15-20 ya wakazi wa Uingereza wameathirika na uvimbe kwenye tumbo. Mara nyingi watu hawagundua ikiwa wana uvimbe wa aina hii na hivyo wengi hawapati matibabu.
Uvimbe wa aina hii unaweza kusababisha kansa ikiwa matibabu hayatatolewa mapema.
- Mkate 'tosti' unaweza kuchangia saratani
- Onyo kuhusu saratani ya matiti bila uvimbe
- Kuenea kwa saratani kumepungua kwa 75% katika vipimo
- Mguu uliokatwa, sasa wapata akaunti ya Instagram
Katika utafiti huu, watafiti walitumia data kutoka kwa wagonjwa 16,600, ambapo iligunduliwa kuwa wagonjwa wenye umri wa miaka 20 hadi 39 ambao walikuwa wametumia dawa za 'antibiotic' kwa miezi miwili au zaidi walikuwa na uwezekano mkubwa wa kupata uvimbe wa tumbo unaojulikana kama adenomas, baadaye maishani, ikiwalinganisha na wenzao wa umri huo ambao hawajatumia dawa za kuzuia magonjwa .
Pia wanawake ambao walikuwa wamemeza dawa hizi kwa miezi miwili au zaidi wenye umri wa miaka 40 hadi 59 walikuwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kupata adenoma siku za usoni.
Watafiti hao wanakiri kuwa utafiti wao hauwezi kudhibitisha kuwa dawa za kuzuia magonjwa husababisha kansa na wanakiri kuwa bacteria ambazo dawa hizi zafaa kuua zaweza pia kuchangia kumea kwa uvimbe wa saratani.
0 Post a Comment:
Post a Comment