Marekani yakatiza ufadhili kwa UNFPA linalohusika na mpango wa uzazi



 marekani yaja na jipya

Mama anamnyonyesha mtotoHaki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGES
Image captionUNFPA huhimiza afya ya uzazi na mpango wa uzazi katika takriban nchi 150 duniani
Marekani imesitisha ufadhili kwa mfuko wa Umoja wa Mataifa wa idadi ya watu, UNFPA unaotoa msaada kwa ajili ya mpango wa uzazi kote duniani.
Hatua hiyo italifanya shirika hilo la Umoja wa Mataifa kupoteza takriban dola milioni thelathini za ufadhili kwa mwaka huu pekee.
UNFPA limepinga madai kuwa linafadhilili shughuli za uaviaji mimba.
Hili ni shirika la kwanza la Umoja wa mataifa kukabiliwa na kupunguwa kwa ufadhili baada ya ahadi ya kupunguza msaada wa kifedha kutoka kwa utawala wa Trump.
Nikki HaleyHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBalozi wa Marekani kwa Umoja wa mataifa Nikki Haley anasimamia uwezekano wa kupunguza ufadhili kwa Umoja huo
Hii ina maana kuwa UNFPA litapoteza ufadhili wa siku zijazo zikiwemo dola milioni 32.5 zilizokuwa zimepangwa kutumiwa mwaka huu.
Wizara ya mambo ya nje Marekani inasema kuwa uamuzi huo ulizingatia shughuli za UNFPA za mpango wake wa uzazi na serikali ya Uchina, ambazo inasema ulisaidia kuavya mimba na kufunga uzazi kwa lzima.
Badala yake ufadhili huo utaelekezwa katika mipango mingine ya uzazi katika nchi zinazoendelea.
Shirika hilo hatahivyo limesema kuwa madai hayo ''si sahihi'', na kwamba kazi zake zote zimekuwa ni za kuboresha haki za kibinfasi na wanandoa kuchukua maamuzi yao bila ubaguzi.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: