Askofu Kakobe akana kukwepa kodi,asema taarifa za TRA ni za Kisiasa

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM=>
Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Followship (FGBF), Zachary Kakobe amekanusha taarifa za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwamba kanisa lake linakwepa kodi.

Akizungumza leo Jumapili Februari 25, 2018 katika kanisa hilo lililopo Mwenge, jijini Dar es Salaam, Baba Askofu Kakobe amewataka waumini wa kanisa hilo kuzikataa taarifa hizo na kwamba zimejaa siasa.


Baada ya TRA kutoa taarifa siku ya Jumanne ya Februari 20, 2018 ikidai ni matokeo ya kiuchunguzi walioufanya baada ya kauli aliyoitoa Askofu huyo mnamo Agosti 2, 2014 kwamba ana pesa nyingi kuliko serikali, "Taarifa hizo zimepotoshwa kwa makusudi au kwa kughafirika" Alisema.

Baba  Askofu Kakobe alisema hakutaka kujibu haraka taarifa hiyo, maana majibu yake yangekuwa habari kubwa na hivyo kulitoa taifa katika mijadara ambayo imekuwapo tangu mwisho wa wiki iliyopita, pia alitaka atoe majibu mbele ya waumini wa kanisa la Full Gospel analoliongoza ambao ndio wadau wa kwanza wa taharifa hiyo. Askofu Kakobe Bible Fellowship.

 Aliendelea kusema "Swali la kujiuliza, kwa nini TRA imeamua kutoa taarifa hiyo sasa? Tena taarifa ambayo imepikwa na si kweli, na lengo kubwa ambalo TRA walikuwa nalo ni kunichonganisha mimi na waumini wangu jambo ambalo ni biashara kichaa"

Baba Askofu Kakobe amesema aliyekuwa anachunguzwa ni yeye lakini ameshangaa kwenda kutolewa ripoti ya kanisa analoliongoza.

Pia Baba Askofu Kakobe aliendelea kutoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja za TRA ikiwemo kwamba kanisa limekwepa kodi, " TRA wakisema mapato yaliyoko kwenye akaunti ya kanisa yanatokana na zaka, changizo na sadaka na hivyo haiwezi kukatwa kodi lakini wanasema kanisa limekwepa kodi, kodi ipi? Kama sio kujichanganya? " Alisema.

Pia ameishangaa ripoti hiyo kudai fedha za kanisa zinatumika kujenga nyumba ya mke wa Kakobe kitu ambacho si kweli, huku akiita ripoti hiyo ingetolewa na Shilawadu ingeleta maana lakini kutolewa na taasisi nzito kama TRA ni jambo la kushangaza sana, huku akitolea ufafanuzi kwamba fedha zinazojenga nyumba hiyo zinatokana na waumini ambao waliamua kujichanga ili waweze kumjengea nyumba mchungaji wao kutokana na nyumba anoyoishi ambayo aliijenga mwaka 1986 kabla ya kuanza kwa kanisa hilo kutokuendana na hadhi ya Askofu huyo, hivyo kwa mapenzi yao walianza kujichangisha tangu mwaka 2009 ili waweze kumjengea nyumba mchungaji wao, na akasema si mara ya kwanza Askofu au mchungaji kujengewa nyumba na waumini wake.

Pia akasema ni kweli alimuandikia barua mheshimiwa Rais na ilikuwa ni barua ya kichungaji na hakupeleka nakala TRA ilikuwa ni ya siri lakini alishangaa barua hiyo kutajwa na TRA, na kusema je TRA imekuwa msemaji wa Rais?Tena barua hiyo haikuwa na mahudhui hayo yaliyotajwa na TRA.

Akaendelea kusema kwamba barua hiyo alikuwa anamweleza Rais kwamba kama vile Isaya alivyotumwa kwa mfalme Hezekia katika ISAYA 38:1 na kuendelea,  Hezekia baada ya kuugua sana aliomba sana kwa Mungu na ndipo Isaya alipotumwa kwa mfalme, na hivyo hivyo Rais amekuwa akisema kila siku aombewe , na hivyo mahubiri yake aliyotoa ibada ya Christmas tarehe 25, Desemba  2017 ni sehemu ya majibu ya maombi anayotaka kuombewa kwamba anapaswa kutubu.

Pia akaendelea kusema Mungu anaposema husema na kila mtu yeye ni kama kinywa tu kinachotumiwa na Mungu hivyo kamwe hawezi kusema neno ambalo hajatumwa na Mungu.

Baba Askofu Kakobe akaendelea kusema kwamba, hajafikia hatua ya kuomba radhi kutokana na kile anachohubiri na kabla hajafikia hatua hiyo ni bora afe. 

Amesema kuomba radhi kwa neno ambalo analifundisha ni kujivua ufalme wa Mungu maana neno la Mungu linasema atakayenionea haya mimi na maneno yangu nami nitamuonea haya mbele za Baba yangu(MARKO 8:38).

Hivyo akasema kama kuomba radhi basi Mungu ndo alitakiwa aombe radhi sio yeye.

Pia akasema serikali isitumie vyombo vya kiserikali kama fimbo ya kuwanyamazisha watu ambao watasema maneno ambayo hayawapendezi watawala, kodi inatakiwa kupendwa na kila mwananchi na isiwe adhabu. Akasema kufanya hivyo ni kupeleka taifa katika ukomunisti ambapo mtu atatakiwa ahubili maneno yanayowapendeza watawala.


Mwisho kabisa akasema amelipa gharama kutokana na injili aliyoihubiri na yupo tayari kulipa gharama yoyote itakayojitokeza kama ipo kutokana na kile alichokihubiri.

Baba Askofu Kakobe ametoa ufafanuzi huo zikiwa zimepita siku nne tangu TRA kutoa taarifa ya uchunguzi katika kanisa hilo na kubaini mambo saba.

Hata hivyo kabla hata ya kutoa ufafanuzi huo waumini wa kanisa la FGBF Tanzania nzima walisema kuwa taarifa za TRA ni uongo mtupu na kusema kwamba kwa jinsi wanavyomfahamu Baba Askofu Kakobe hawezi kukemea dhambi halafu akaipaka rangi baadaye kwa kusema kuwa alitamka maneno ya kebehi.

Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: