Ndassa ataka Uwanja wa Taifa utumike kwa utalii





UWANJA wa Taifa utumike kama kivutio cha utalii kwa kualika timu kubwa na wachezaji wenye majina kuja kucheza na baadaye watembelee mbuga za wanyama na kuongeza kipato. Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa (CCM) alitoa hoja hiyo jana bungeni mjini hapa alipouliza swali la nyongeza kuhusu mkakati wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuhusu kuongeza matumizi ya uwanja huo.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura alikubali wazo hilo na kwamba serikali itakwenda kulifanyia kazi. “Wazo lako ni jema na tumelipokea na tutakwenda kulifanyia kazi,” alisema. Ndasa alitoa kauli kutokana na uzoefu wake, kutokana na baadhi ya timu kualikwa na kutembelea nchini, nchi ilifaidika kwa mapato ya uwanjani na kwenye vivutio vya utalii.
Mfano wakati ilipotembelea Brazil, nchi ilipata faida kubwa kutokana na kuingia kwa timu hiyo katika mchezo lakini pia timu ilitembelea vivutio na kuchangia pato kwenye utalii. Brazil ilitembelea nchini mwaka 2010 ikipita kwenda Afrika Kusini kwenye kombe la dunia ambapo ilicheza mechi ya kirafiki na Taifa Stars na kuifunga mabao 5-1. Kutembelea kwa timu hiyo serikali ilipata mapato kutokana na timu kucheza lakini pia kutembelea mbuga na hifadhi zetu na wakaongeza la utalii nchini.


                        like, comment and share
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: