Meli kubwa ya Kijeshi inayomilikiwa na jeshi la Marekani, imewasili na kutia nanga katika Pwani ya Korea Kusini.
Meli hiyo iitwayo, USS Michigan, imeongeza wasiwasi kutokana na Marekani na Korea Kaskazini kujibizana vikali na kutoleana vitisho katika siku za karibuni.
Nyambizi ya USS Michigan hutumia nguvu za nyuklia na hubeba makombora aina 154 na wanajeshi 60 pamoja na meli nyambizi nyingine ndogo, gazeti la Korea Kusini la Chosun Ilbo limeripoti.
Meli hiyo inatarajiwa kushiriki kwenye mazoezi ya kijeshi pamoja na kundi la meli zinazoongozwa na Carl Vinson, kundi ambalo lilitumwa eneo la Korea kuonyesha ubabe wa kijeshi wa Marekani.
0 Post a Comment:
Post a Comment