Mchezaji nyota wa mabingwa watetezi mpira wa wavu Jeshi Stars (wanaume), Nassoro Sharifu ametamba kuwa wamejipanga kutetea taji lao baada ya kushinda michezo mitatu mfululizo.
Jeshi Stars imesaliwa na michezo miwili kabla ya hatua ya nusu fainali wanaonekana kuwa na nafasi kubwa kutinga hatua hiyo kutokana na kuwafunga Magereza kwa seti 3-1, Polisi 3-1 na Moro Stars 3-0.
"Tunachotaka ni kuongoza Kundi A ili tucheze na timu itakayoshika nafasi ya pili kutoka Kundi B, tume kuwa tukicheza kila mchezo kwa umakini ndio maana tumeweza shinda mechi zote.
"Lengo letu ni kutetea ubingwa kwa kuwa tunajua kuwa bingwa ndiye atakaye shiriki mashindano ya klabu bingwa Afrika mwakani" alisema Nassoro.
Mchezaji huyo amekili kuwepo na ushindani wa aina yake kwenye mashindano hayo tofauti na misimu kadhaa nyuma.
comment, like and share
0 Post a Comment:
Post a Comment