THURSDAY, APRIL 6, 2017
Operesheni ya Takukuru yaokoa Sh9bilioni
Dodoma. Serikali imeokoa Sh9.75 bilioni katika mwaka wa Fedha 2016/17 kutokana na operesheni zilizofanywa na Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema hayo leo wakati akisoma bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Bunge kwa Mwaka wa Fedha 2017/18 bungeni.
Amesema katika Mwaka wa fedha 2017/18 Serikali itaendelea na mapambano yake dhidi ya rushwa hususan katika eneo la ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
"Kudhibiti mqtumizi ya fedha za umma na malipo hewa na kuimarisha ufuatiliaji na ukaguzi wa miradi ya maendeleo," amesema
Majaliwa amesema katika Mwaka wa Fedha 2016/17, Takukuru imefanya uchunguzi wa majalada 306 ya tuhuma za rushwa na kupata kibali cha Mkurugenzi wa Mashtaka nchini kuendelea na mashtaka kwa majalada 104.
0 Post a Comment:
Post a Comment