Waarabu wamsifu 'Abu Ivanka' almaarufu rais Donald Trump kwa mashambulizi dhidi ya Syria
Waarabu wamsifu 'Abu Ivanka' almaarufu rais Donald Trump kwa mashambulizi dhidi ya Syria
Waarabu katika mitandao ya kijamii wamem'miminia sifa tele rais wa marekani Donald Trump na shukrani na shangwe baada ya kuamrisha shambulizi la kwanza la kijeshi kutoka Marekani dhidi ya vikosi vya serikali ya Syria.
Marekani ilifanya mashambulizi hayo dhidi ya kambi ya jeshi la wanahewa katika majira ya asubuhi siku ya Ijumaa kufuatia shambulizi linalokisiwa kuwa la kemikali katika jiji linaloshikiliwa na waasi.
- Trump: Clinton ataanzisha Vita Vikuu vya Dunia
- Rubani wa ndege ya jeshi la Syria iliyoanguka apatikana
- Trump: Wakimbizi wa Syria hawaruhusiwi Marekani
Muda mfupi baadaye, baadhi ya Waarabu wanaotumia mitandao ya kijamii walianza kumtaja Rais Trump kama 'Abu Ivanka' - au babake Ivanka, kama onyesho la heshima kwake
Wengine walimuita Abu Ivanka al-Amreeki - au babake Ivanka Muamerika, akiwa amefuga ndevu.
Lakini kuna wale walioshuku mwelekeo wa rais huyo na nia yake.
Mtumizi mmoja alimpa Trump sura mpya akitumia picha yake akiwa amevalia kofia ya utamaduni iitwayo tarboosh, na maandishi: " Tunakupenda"
Pia alitajwa kama mtu anayesema na kutenda, huku mtumizi mmoja akimuambia alifanya kwa muda mfupi kile Obama hakuweza timiza kwa miaka minane.
"ndege kumi na tano za kijeshi ambazo zingewaangamiza maelfu ya wakaazi wa Syria" zimeharibiwa, mtumizi mmoja alisema, huku akibadilisha picha yake kwa mtandao wa facebook na kuweka sura ya Trump, bendera ya Marekani na maandishi ya kiarabu: '' Tunakupenda"
- Marekani imeishambulia Syria kwa makombora.
- Mshirika wa Osama auawa Syria
- Marekani yapokea mkimbizi toka Syria
Mwanaharakati wa wanahabari kutoka Idlib alitaka kuona hatua ikiendelea kuchukuliwa, akimuita rais wa Marekani aendelee na kuipiga vita Assad.
Huku wengine wakisema kuwa hawangedhania siku hii ingefika, walimshukuru Trump kwa kufanya kile viongozi waoga wa Kiarabu hawangeweza kufanya.
"Matumaini yanarejea pole pole mioyoni mwetu. Asante Trump," Msyria mmoja alisema.
Kwa mara ya kwanza kwa miaka sita, serikali ya Assad imewajibika kwa vitendo vyao vya uhalifu," raia mwemgine wa Syria anayeishi mjini London alisema.
Msyria mwengine kutoka Houston pia alisambaza picha ya kuashiria mapenzi kwa rais wa Marekani.
Mwanahabari kutoka Syria Rami Jarrah alikuwa na maoni tofauti kidogo akisema kuwa wenyeji wa Syria hawamfurahii mtu kama Trump, wana furaha tu kuwa Assad amepunguziwa njia za kuwauwa"
Wengine walishuku lengo la Trump: " Hivi mwafikiri Trump aliishambulia Assad kwa sababu ya upendo kwa walionusurika? Tumekuwa tukikabiliana na mauaji ya watu wengi, mabaya hata kuliko ya Wayahudi na leo dhamira ya Marekani na dunia nzima ndio imeamka?"
"Trump amegundua siri ya siasa za Marekani: Vitu vikienda mrama nyumbani, anzisha mradi wa kijeshi mashariki ya kati," alisema mwandishi katika mitandao ya kijamii Karlo Sharro.
Mwingine akaongezea, " Kwa hivi sasa mwampenda Trump? Wako wapi wale waliosema anawachukia Waarabu na Waislamu alipochukua mamlaka?"
0 Post a Comment:
Post a Comment