UN yafuatilia kumbukumbu za kimbari
Ofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Idara ya Ushirikiano wa Nchi za Nje,
Nguse Nyerere alisema jukumu la ulinzi na amani ya nchi, linamhusu kila
raia siyo la jeshi la kulinda amani.
“Jambo la msingi ni kutunza amani kwa sababu majeshi ya kulinda amani
hayasaidii sana, ndiyo maana hata wanajeshi wa Ubelgiji waliondoka Rwanda
wakati hali ikiwa tete, lakini kama raia wa Rwanda wangelinda amani yao
mambo yote yasingetokea,” alisema Nyerere.
Ofisa Habari wa UN, Stella Vuzo aliwataka vijana wote nchini kutokubali
kutumiwa kuua wenzao kwa sababu watu wote ni sawa, licha ya tofauti na
upungufu uliopo kwa kila mmoja au jamii.
Pia, Vuzo alisoma ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja UN, Antonio Guterres ambao unasema: “Njia pekee ya kuwakumbuka waliouawa nchini Rwanda, ni kuhakikisha matukio kama hayo hayatokei tena.
Dunia lazima iwe macho daima na viashiria vya mauaji ya kimbari na kuchukua hatua za haraka na mapema dhidi ya tishio hilo.”
Mwanafunzi Caroline Augastino wa kidato cha sita Sekondari ya Kibasila, alisema kupitia maadhimisho hayo amejifunza umhimu wa kutunza amani ya nchi.
“Kama Watanzania tunapaswa kutoruhusu sababu ndogondogo zikatugawa kama ilivyotokea kwa wenzetu Rwanda, kwa sababu ukiachilia mbali tofauti zilizopo binadamu wote ni sawa,” alisema Caroline.
Wanafunzi waliohudhuria kumbukumbu hiyo ni kutoka sekondari za Kibasila, Wailes, Airwings, Tirav, Miburani, Kigamboni na vijana kutoka vikundi vya Temeke Youth Development Network (Teyoden) na Kigamboni Youth Network (Kipnet).
Mauaji ya Kimbari ya Rwanda yalikuwa ya halaiki mwaka 1994; yakihusisha kabila la Watusi na Wahutu licha ya kudumu takriban siku 100, inakadiriwa watu 500,000 waliuawa, au karibu asilimia 20 ya idadi ya wat
0 Post a Comment:
Post a Comment