Watu wanne kizimbani kwa kujipatia Sh 700 milioni za udanganyifu

Watu wanne kizimbani kwa kujipatia Sh 700 milioni za udanganyifu 


 Dar es Salaam. Watu wanne wamepandishwa kizimbani  katika Mahakama ya Kisutu na kusomewa mashtaka matatu likiwamo la  kula njama, kutakatisha fedha na kujipatia USD 320,000 kwa njia ya udanganyifu ambazo ni sawa na Sh 704 milioni.
Akiwasomea hati ya  mashtaka leo, Wakili wa Serikali, Esterzia Martin  kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Deogratius Masika(40), William Kimonge (34), Yusuph Sabo (27) na Elladius  Tesha (47).
Wakili huyo amedai kuwa kati ya Oktoba  2016 na Januari 2017 jiji Dar es Salaam washtakiwa hao walikula njama ya kutenda makosa ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Alidai kuwa kati ya Desemba 2016 na Januari 2017 washtakiwa hao walipatia USD 320,000 ambazo ni sawa na Sh 704 milioni  baada  kujifanya watasambaza tani 5,000 za Korosho kutoka Mtwara kupitia kampuni ya SMCI America LLC ambayo ipo Marekani wakati wakijua ni uongo.
  
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: