Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ametoa uamuzi huo baada ya kusikiliza pande zote mbili.
Hakimu Mashauri amesema Joram Bashange ambaye aliapa katika kiapo kuwa ni Katibu wa Bodi ya Wadhamini ya CUF aliapa uongo kwa sababu bodi hiyo ilikwisha muda wake.
Hivyo, Bashange kuwa ni Katibu wa Bodi ya Wadhamini ya CUF ni uongo na kwamba yeye binafsi atabeba gharama za kesi.
Katika kesi hiyo Sakaya na wenzake walikuwa wakiwakilishwa na Wakili, Mashaka Ngole huku bodi ya wadhamini ya CUF ikiwakilishwa na Wakili Hashimu Mziray.
0 Post a Comment:
Post a Comment