24 Mei 2017
Mamia ya watu wamejitokeza kuzunguka nyumba lilipotokea tukio hilo baada ya kuona moshi ukitoka katika moja ya chumba na kuonekana miili ikiwa imeteketea kwa moto.
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha,Charles Mkumbo alisema tuki hilo lilitokea jana, Jumanne saa 3.00 asubuhi
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha,Charles Mkumbo alisema tuki hilo lilitokea jana, Jumanne saa 3.00 asubuhi
Amesema aliyekutwa amefariki ni Maurine Urio (32) pamoja na rafiki yake huyo ambaye hajaweza kutambulika kutokana na kuungua sana.
“Tumepata taarifa asubuhi hii kuwa kuna nyumba inaungua na polisi pamoja na zimamoto walifika eneo la tukio na kukuta watu hao wameshapoteza maisha wakiwa juu ya godoro ambako mwanaume alionekana kabla ya kuchomwa alifungwa kamba miguu na mikono ili kuzibitiwa,”alisema.
Mkumbo alisema miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa Mount Meru huku wahusika wa tukio hilo wakiwa wanatafutwa.
Akizungumzia tukio hilo mwenyekiti wa mtaa wa Ilkiurei iliyoko kata ya Kiranyi, Onesphory Chami amedai kuwa tukio hilo linahusishwa na wivu wa mapenzi.
0 Post a Comment:
Post a Comment